Pata taarifa kuu

Uvujaji wa hati zilizoainishwa waisumbua Pentagon

Uvujaji wa nyaraka za siri za Marekani, hasa zinazohusiana na Ukraine na ambazo zinaonekana kuwa halisi kwa sehemu kubwa, zinasababisha hatari 'kubwa zaidi' kwa usalama wa taifa wa Marekani, Pentagon imetangaza. 

Makao makuu ya CIA huko Langley.
Makao makuu ya CIA huko Langley. AP - J. Scott Applewhite
Matangazo ya kibiashara

Ukweli kwamba hati hizi zinasambazwa mtandaoni ni "hatari kubwa kwa usalama wa taifa na zina uwezo wa kuchochea habari potofu", msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Chris Meagher, amewaambia waandishi wa habari.

“Tunaendelea kuchunguza jinsi hili lilivyotokea, pamoja na ukubwa wa tatizo, hatua zimechukuliwa ili kuchambua zaidi namna taarifa za aina hii zilivyosambazwa na kwa nani,” ameongeza.

Mtiririko thabiti wa picha za hati zilizoainishwa zimegunduliwa kwenye Twitter, Telegraph, Discord na tovuti zingine katika siku za hivi karibuni, ingawa zingine zinaweza kuwa zimesambazwa mtandaoni kwa wiki kabla ya kuvutia umakini wa vyombo vya habari.

Msemaji wa Pentagon alikataa kuzungumzia kuhusu ukweli wa hati hizi, akisema timu ya wizara ilikifanya kazi kubaini kama walikuwa au la, lakini alibainisha kuwa picha zilizotolewa zilionekana kuwa na habari nyeti.

"Picha zinaonekana kuonyesha hati katika muundo sawa na ule unaotumiwa kutoa sasisho za kila siku kwa shughuli zetu kuu zinazohusiana na Ukraine na Urusi, pamoja na sasisho zingine za kijasusi," amesema, lakini zingine "zinaonekana kuwa zimehaririwa. "

Angalau hati moja inaonekana kubadilishwa ili kupendekeza kwamba Ukraine ilipata hasara kubwa kuliko Urusi, wakati ile iliyodhaniwa ya awali ilisema kinyume.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.