Pata taarifa kuu

Argentina: Kukatika kwa umeme kumeathiri mamilioni ya familia huku kukiwa na joto kali

Mamilioni ya watu hawakuwa na umeme kwa angalau saa mbili Jumatano Machi 1 nchini Argentina. Wakati nchi hiyo kwa sasa inapitia wimbi kubwa la joto, karibu nusu ya eneo la Argentina imeathiriwa na kukatwa kwa umeme. Mwanzoni mwa kukatika huku, moto katika jimbo la Buenos Aires ambao uliathiri majimbo ya kati na kaskazini-magharibi, kama vile Cordoba, Santa Fe, Mendoza, na sekta fulani za mkoa wa Buenos Aires.

Raia wa Argentina wanasubiri katika kituo cha treni cha Constitucion huko Buenos Aires mnamo Machi 1, 2023, wakati kukitokea hitilafu kubwa ya umeme.
Raia wa Argentina wanasubiri katika kituo cha treni cha Constitucion huko Buenos Aires mnamo Machi 1, 2023, wakati kukitokea hitilafu kubwa ya umeme. © Luis Robayo / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ilikuwa ni baada ya saa kumi jioni Jumatano huko Buenos Aires wakati taa za barabarani zilipoacha kufanya kazi, na kusababisha fujo katika mitaa ya mji mkuu wa Argentina. Vitongoji vyote havina umeme, na hivi karibuni imefahamika kwamba kukatwa kwa umeme kwa kweli kunaathiri angalau majimbo 11 kati ya 24 ya nchi, yaani karibu nusu ya eneo la Argentina.

Hakuna ripoti rasmi

Ikiwa hakuna ripoti rasmi iliyowasilishwa jioni, vyombo vya habari vya ndani viliweka mbele idadi ya watu milioni 20 walioathirika kwa saa kadhaa. Kulingana na Naibu Katibu Mkuu wa Nishati wa Argentina, chimbuko la kukatika huku lilikuwa moto karibu na njia za umeme wa juu, ambao ungesababisha mfululizo wa matukio ya kuporomoka kwenye gridi ya taifa ya umeme.

Mipasuko hii basi ingesababisha kuzimwa kiotomatiki kwa kinu cha nyuklia cha Atucha kama hatua ya usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.