Pata taarifa kuu

Pele akabiliwa na ugonjwa hatari wa Saratani na 'figo na moyo vyashindwa kufanya kazi'

Saratani ya Pele "inaendelea" na nguli huyo wa soka wa Brazil anahitaji "huduma zaidi" kutokana na "figo na moyo kushindwa kufanya kazi", imetangaza hospitali ya Sao Paulo ambako binti zake walikuwa wakijiandaa kusherehekea Krismasi siku ya Jumatano.

Mwanasoka wa zamani wa Brazil Pelé, huko New York, katika majengo ya shirika la habari la AP.
Mwanasoka wa zamani wa Brazil Pelé, huko New York, katika majengo ya shirika la habari la AP. © AP - Mark Lennihan
Matangazo ya kibiashara

"King" Pelé, 82, alilazwa katika Hospitali ya Albert Einstein mnamo Novemba 29 kwa tathmini ya matibabu yake baada ya kugunduliwa kwa tumor ya koloni mnamo Septemba 2021.

"Mgonjwa ana dalili za kuendelea kwa ugonjwa na anahitaji uangalizi mkubwa zaidi ili kushughulikia tatizo la kushindwa kwa figo na moyo," madaktari wanaeleza katika taarifa yao ya afya.

Mbrazil huyo bado amelazwa hospitalini "katika chumba cha kawaida, ambapo anapata huduma muhimu", hospitali hiyo imeongeza.

Dakika chache kabla ya kuchapishwa kwa taarifa hii kwa vyombo vya habari, mabinti wawili wa Pelé, Kely Nascimento na Flavia Arantes, walitangaza kwenye kurasa zao za Instagram kwamba baba yao atasheherekea Krismasi hospitalini.

"Krismasi yetu nyumbani haitasheherekewa. Tumeamua na madaktari, kwamba kwa sababu mbalimbali, ni bora kukaa hapa, pamoja na huduma zote zinazotolewa na familia yetu mpya (kutoka hospitali ya Albert) Einstein", imeandikwa kwenye ujumbe huu,  wenye picha ya dada hao wawili wanaotabasamu.

Wasichana hao wawili wamechapisha jumbe kadhaa kwenye mitandao ya kijamii katika wiki za hivi karibuni ili kuwatuliza mashabiki wa Pele kote ulimwenguni, baada ya vyombo vya habari vya Brazil kuripoti kuwa afya yake ni mbaya.

Siku ya Jumapili, Kely Nascimento alichapisha picha ya dadake Flavia akikanda mguu wa kushoto wa babake alipokuwa akitazama fainali ya Kombe la Dunia kwenye televiseheni. Uso wa Pele hauonekani kwenye picha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.