UFARANSA-MAREKANI
Macron awasili nchini Marekani, kukutana na mwenyeji wake Biden
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amewasili nchini Marekani kukutana na mwenyeji wake Joe Biden, ambapo viongozi hao wawili watazungumzia ushirikiano na namna ya kuimarisha biashara, masuala ya usalama kati ya nchi zao, bila kusahau vita vinavyoendelea nchini Ukraine.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
John Kirby msemaji wa Ikulu ya Marekani anayehusika na masuala ya usalama wa kitaifa, hapa anaeleza ni kwanini rais Biden ameamua kumwalika rais Macron kama kiongozi wa Kwanza wa kigeni, katika kipindi hiki cha uongozi wake.
Namna rais Biden anavyoshughulikia sera yake ya mambo ya nje, ni kuimarisha ushirikiano wake na washirika wake, kama Ufaransa ambaye ni mshirika wa muda mrefu.
Baada ya kuondoka jijini Washington DC, Macron anatarajiwa kutembelea New Orleans, êneo ambalo lina wakaazi wengi wa Ufaransa.