Pata taarifa kuu

Marekani: Joe Biden ataka "kutathmini upya" uhusiano wake na Saudi Arabia

Joe Biden anataka "kutathmini upya" uhusiano wa Marekani na Saudi Arabia, Ikulu ya Marekani imesema siku ya Jumanne. Tangazo hilo linafuatia tatatizo la kidiplomasia kwa uamuzi wa OPEC+ wiki iliyopita wa kupunguza viwango vyake vya uzalishaji wa mafuta.

Rais wa Marekani Joe Biden alisafiri hadi Jeddah, Saudi Arabia, Julai 2022 kwa ziara rasmi.
Rais wa Marekani Joe Biden alisafiri hadi Jeddah, Saudi Arabia, Julai 2022 kwa ziara rasmi. AFP - BANDAR AL-JALOUD
Matangazo ya kibiashara

Mnamo mwezi wa Julai, rais wa Marekani alikwenda Riyadh kukutana na mwana mfalme ambaye aliapa nchi yake kuendeleza uhusiano na Marekani.

Athari ya moja kwa moja ya udhalilishaji wa kidiplomasia aliyopata Joe Biden wiki iliyopita, kupeana mkono na Mohamed ben Salman ambako ilitafsiriwa kuwa alipigwa kofi usoni, kama vyombo vya habari vya Marekani vinavyoandika.

wiki iliyopita, OPEC+ ilitangaza kwamba itapunguza uzalishaji wake wa mafuta. Kashfa kwa Ikulu ya Marekani ambayo inajibu leo. "Rais amekuwa wazi, alisema msemaji wake John Kirby, lazima tutathmini upya uhusiano huu" na Saudi Arabia. Naye Joe Biden anasema yuko tayari kutafakari upya uhusiano huu kwa ushirikiano na Congress, wakati ambapo maafisa kadhaa waliochaguliwa wenye ushawishi mkubwa wanatoa wito wa kukomesha kuiuzia silaha ufalme wa Saudi arabia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.