Pata taarifa kuu

Rapa wa Marekani Coolio afariki akiwa na umri wa miaka 59

Rapa wa Marekani Coolio, anayefahamika zaidi kwa kibao chake cha "Gangsta's Paradise" kilichotolewa mwaka wa 1995, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 59, meneja wake alitangaza Jumatano.

Rapa Coolio, hapa wakati wa 'I Love the 90's Tour' mnamo Agosti 7, 2022 huko Aurora, Illinois.
Rapa Coolio, hapa wakati wa 'I Love the 90's Tour' mnamo Agosti 7, 2022 huko Aurora, Illinois. © Rob Grabowski/Invision/AP
Matangazo ya kibiashara

Jina lake halisi ni Artis Leon Ivey Jr, mwanamuziki aliyetunukiwa tuzo ya heshima ya Grammy alifariki huko Los Angeles, kulingana na taarifa za meneja wake Jarez Posey wakati akizungumza na shirika la habari la Ufaransa AFP. Hata hivyo hakueleza sababu za kifo chake.

Meneja huyo, pia ambae ni rafiki wa karibu na wa siku nyingi wa rapa huyo, aliiambia TMZ - chapisho maalumu kwa habari za watu mashuhuri - kwamba alimkuta akiwa amepoteza fahamu kwenye bafu la rafiki yake.

Coolio alianza uchezaji wake huko California mwishoni mwa miaka ya 1980, lakini akaibuka na umaarufu na "Gangsta's Paradise" ya 1995, ambayo iliangaziwa kwenye wimbo wa filamu "Rebellious Minds."

Wimbo huo ulimpa tuzo ya Grammy mwaka uliofuata.

Alichukua kiitikio cha muziki wa "Pastime Paradise", wimbo wa Stevie Wonder uliotolewa mwaka 1976.

Kichocheo hicho kilikuwa kimeshinda, mamilioni ya nakala za "Gangsta's Paradise" zikitiririka kote ulimwenguni, na kupanda juu ya mauzo katika baadhi ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.