Pata taarifa kuu

Mkutano Mkuu wa UN: Viongozi 150 wakutana wakati dunia yakabiliwa na migogoro mbalimbali

Wiki hii macho yataelekezwa mjini New York, ambapo marais na wakuu wa serikali 150 wanakutana na kila mmoja kuhutubia wakati dunia inakabiliwa na mgogoro mkubwa, ukihusishwa hasa na vita nchini Ukraine. Mkutanokuhusu elimu utafanyika kwanza, lro Jumatatu Septemba 19, na kuanzia Jumanne marais na wakuu wa serikali watapishana kwenye jukwa la Umoja wa Mataifa.

Mbele ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa, huko New York, Septemba 16, 2022.
Mbele ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa, huko New York, Septemba 16, 2022. AP - Mary Altaffer
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu mkuu unawaleta pamoja viogozi wa dunia ambao watakutana uso kwa uso na kisha kila mmoja kuhutumbia mkutano huo. Katika miaka miwili iliyopita, kwa sababu ya janga la UVIKO-19, sehemu ya hotuba zilizorekodiwa zilifanywa kwa njia ya video.

Bado kutakuwa na hotuba zilizorekodiwa mwaka huu: ile ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, iliyoidhinishwa na kura maalum. Urusi bila shaka ilipinga.

Vladimir Putin na Xi Jinping kutohudhuria

Rais wake Vladimir Putin, kama mwenzake wa China Xi Jinping hawatahudhuria mkutano huo wa wiki hii. Ni wazi kwa upande wao mkutano wa muhimu na bora, ulikuwa wa wiki iliyopita uliowakutanisha Samarcande ambao ulileta pamoja nchi kadhaa zinazopinga Marekani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alilaani siku chache kabla ya Mkutano Mkuu, mgawanyiko katika umoja huo "ambao haujawahi kushuhudiwa tangu Vita Baridi", alitoa wito "kukutana" kupatiwa suluhisho "changamoto kubwa".

Ukraine, mgogoro wa nishati na tabia nchi kwenye ajrnda ya mkutano

Kati ya changamoto ambazo viongozi wa dunia watajadili, bila shaka ni pamoja na vita nchini Ukraine. Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umepangwa Alhamisi, wakati baadhi ya nchi za kusini zinaghadhabishwa kwamba nchi za Magharibi zinajihusisha na mzozo huu.

Changamoto zingine: Mgogoro wa kiafya wa UVIKO-19, mgogoro wa nishati ambayo inatishia Ulaya, na mabadiliko ya tabia nchi, miezi miwili kabla ya mkutano wa COP 27 nchini Misri na wakati mafuriko yanaathiri theluthi moja ya Pakistan. Siku ya Jumatano, mkutano umepangwa kuhusiana na suala hilo. Pia kufuatia mkutano wa kilele wa ECOWAS pembeni mwa Mkutano Mkuu, kutajadiliwa juu ya Mali inayovutana na Côte d'Ivoire.

Antonio Guterres amesema kikao chake cha kwanza cha mkutano huu lo Jumatatu Septemba 19,  kitajikita katika elimu, lakini kutakuwa na viongozi wachache kuliko ilivyotarajiwa kwa sababu ya mazishi ya Malkia upande wa pili wa Atlantiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.