Pata taarifa kuu

Wauguzi 15,000 waingia katika mgomo wa siku tatu kaskazini mwa Marekani

Baadhi ya wauguzi 15,000 katika hospitali 16 huko Minnesota na Wisconsin wamesitisha kazi kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi asubuhi. Wagomaji wanadai mishahara bora na rasilimali watu zaidi katika hospitali.

Wauguzi wakifanya maandamano nchini Marekani, Julai 15, 2020.
Wauguzi wakifanya maandamano nchini Marekani, Julai 15, 2020. REUTERS/Octavio Jones
Matangazo ya kibiashara

Huu ni "mgomo mkubwa zaidi wa wauguzi wa sekta ya kibinafsi kuwahi kuandaliwa nchini," kinasema Chama cha Wauguzi cha Minnesota (MNA), ambacho kinaandaa harakati hizo. Jumatatu hii, hospitali kumi na tano katika eneo la Minneapolis zimeathirika.

Ili kudumisha mwendelezo wa huduma, hospitali zimelazimika kuajiri wafanyikazi wa muda na kusema kwamba usumbufu unaowezekana unatarajiwa. Kwa upande wao, wauguzi hao wanasema wataacha kufanya kazi kwa siku tatu, lakini sio kwa muda usiojulikana, ili, kulingana na wawakilishi wao, wasiathiri matibabu ya wagonjwa.

Wanahamasisha hasa kupata mishahara bora na wafanyakazi wa ziada. Lakini pia wanadai kuwa na sauti katika shirika la kazi na usambazaji wa waajiri wowote wapya. "Hivi sasa huko Minnesota, wauguzi wana kazi nyingi, hospitali hazina wafanyikazi, na wagonjwa wanazidiwa," MNA ilisema katika taarifa.

Wauguzi wanadai ongezeko la 27% hadi 30%

Muungano huo unasema unataka kutafuta suluhu kwa matatizo ya upungufu wa wafanyakazi wakati wasimamizi wa hospitali wanataka tu kuzingatia mishahara.

Kulingana na taarifa ya pamoja kutoka kwa viongozi wa hospitali kadhaa zilizoathiriwa, "chama cha wafanyakazi kilikataa maombi yote ya upatanishi na kushikilia madai ya mishahara yasiyo ya kweli, yasiyofaa na yasiyoweza kumudu". Anadai kuwa amependekeza nyongeza ya mishahara kuanzia 10% hadi 12% kwa miaka mitatu, wakati wauguzi wanaomba 27% hadi 30%.

Nchini Marekani, idadi ya wafanyakazi wa afya bado haijarejea katika viwango vya kabla ya janga. Bado kuna 37,000 waliopotea katika ngazi ya kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.