Pata taarifa kuu
HAKI-UCHUMI

Donald Trump akaa kimya wakati akihojiwa kuhusu madai ya udanganyifu wa kodi

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesikilizwa Jumatano hii, Agosti 10 na Mwanasheria Mkuu wa New York kama sehemu ya uchunguzi wa kiraia kwa tuhuma za udanganyifu wa kifedha katika ya kampuni yake kubwa ya Trump Organization.

Donald Trump kabla ya kusikilizwa na Mwanasheria Mkuu wa New York, Agosti 10, 2022.
Donald Trump kabla ya kusikilizwa na Mwanasheria Mkuu wa New York, Agosti 10, 2022. AP - Julia Nikhinson
Matangazo ya kibiashara

Akisikizwa chini ya kiapo na Mwanasheria Mkuu wa New York Letitia James, Donald Trump alikataa kujibu maswali yake kwa tuhuma za udanganyifu wa kifedha ambayo yanamlenga yeye na watoto wake, Ivanka na Donald Jr. Rais wa zamani wa Marekani amejitetea akitaja  Ibara ya 5 ya Katiba ya Marekani, ambayo inabaini kutotoa ushahidi kuhusu madai yanayokuhusu. Katika taarifa yake, Donald Trump amesema kwa mara nyingine tena kuwa analengwa na madai yasiyokuwa na msingi na amedai kuwa "amekataa kujibu maswali, chini ya haki na sheria zilizotolewa na Katiba ya Marekani kwa kila raia".

Alipofika tu katika afisi ya Letitia James, mwanasheria mteule kutoka jamii ya Wamarekani wa Chama cha Democratic, bilionea huyo wa chama cha Republican amedhihaki kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kuhusu "ofisi yake ya kifahari, nzuri na ya gharama kubwa (...) akifanya kazi katika mazingira mazuri wakati watu wwanauawana huko New York na anatumia wakati wake na kujaribu kumkamata Trump."

Trump ataja "utawala wa kibabe" unaoongozwa na Joe Biden

Akiwasili Jumanne jioni katika mji mkuu wa kiuchumi na kitamaduni wa Marekani, mfanyabiashara huyo alitangaza kwamba ataenda "kumuona Mwanasheria Mkuu wa New York mwenye ubaguzi wa rangi". Anaona yeye, pamoja na kampuni yake ya Trump Organisation kwa "ameshambuliwa kutoka pande zote" katika nchi inayotawaliwa na mpinzani wake Joe Biden. "Utawala wa kibabe" kulingana na Donald Trump. Mmoja wa watoto wa Trump, Eric, pia ameshutumu kwenye ukurasa wake wa Twitter ukweli kwamba babake alilazimishwa kutoa "ushahidi mbele ya mawakili wa serikali fisadi zaidi wa Marekani". "Uovu" usiokubalika amesema Eric Trump.

Letitia James aliomba kwa miezi kumsikiliza Donald Trump kuhusu malipo ya kodi kwa kampuni zake na alikuwa alipangwa kusikilizwa Julai 15. Lakini kifo cha mke wa kwanza wa Donald Trump, Ivana, kilisababisha kuahirishwa kwa kesi hiyo. Hatimaye Trump na familia yake walikubali shinikizo baada ya uchunguzi wa miaka mitatu wa mwendesha mashtaka. Kulingana na kituo cha televisheni cha Marekani CNN, Ivanka na Donald Jr walikuwa wamesikilizwa na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mwishoni mwa mwezi wa Julai na mwanzoni mwa mwezi wa Agosti.

Uchunguzi wa kiraia dhidi ya kampuni ya familia ya Trump Organization ulifunguliwa baada ya ushahidi wa kuzuka ghasia katika Bunge la Congress huko Washington na mmoja wa mawakili wa zamani wa Donald Trump, Michael Cohen, akidai tathmini za udanganyifu kwa shughuli za kampuni ya Trump Organization, ili kupata mikopo, kupata punguzo la kodi au fidia bora ya bima.

Letitia James alihakikisha mnamo mwezi wa Januari kwamba "aligundua ushahidi muhimu unaoonyesha kuwa Donald Trump na kampuni ya Trump Oganization walithamini kwa uwongo na kwa udanganyifu mali kadhaa", hasa viwanja vya gofu, madai ambayo yamefutiliwa mbali na mawakili wa Donald Trump.

Mwanasheria Mkuu wa serikali hana uwezo wa kumfungulia mashtaka Donald Trump, lakini anaweza kuanzisha kesi za madai ya kiraia, ikiwa ni pamoja na kutozwa faini kwa uharibifu wa kifedha. Madai hayo pia ni mada ya uchunguzi wa jinai unaoongozwa na mwendesha mashtaka wa Manhattan Alvin Bragg.

Kesi hiyo inakuja siku mbili baada ya msako ambao haujawahi kushuhudiwa katika nyumba ya Donald Trump huko Mar-a-Lago, Florida, na kuzua hasira miongoni mwa Warepublican.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.