Pata taarifa kuu
NATO-MAREKANI

Rais Biden aionya Urusi, aiomba dunia isimame na Ukraine

Wizara ya Ulinzi ya Urusi inasema imeondoa wanajeshi wake katika kisiwa kilichofahamika kama Snake, katika Bahari nyeusi kama ishara ya kuonesha nia ya kuonesha kuwa Moscow inaunga mkono jitihada za kusafirishwa kwa chakula kilichokwama katika bandari za Ukraine.

Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden © Kevin Lamarque / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imesifiwa na serikali ya Ukraine inayosema, ni ushindi mkubwa kwa vikosi vyake vinavyoendelea kupambana na wanajeshi wa Urusi.

Katika hatua nyingine, mkutano wa viongozi kutoka nchi za Jumuiya ya majeshi ya nchi za Magharibi NATO umemalizika jijini Madrid na viongozi kuapa kuendelea kusimama na Ukraine.

Rais Joe Biden ameionya Urusi kutothubutu kuivamia nchi mwanachama wa NATO kwa sababu jeshi hilo lipo imara.

"Tumesisitiza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha tano cha NATO, kinasalia thabiti, yeye anayeshambulia mmoja wetu, tutamshambulia," amesema.

Aidha, ametaka dunia kuendelea kusimama na Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi.

"Marekani inaiomba dunia, kusimama na Ukraine," ameelezea akizungmza jijini Madrid.

Mkutano huu umeikubali nchi ya  Sweden na Finland kuwa mwanachama mpya wa NATO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.