Pata taarifa kuu

Marekani yataka kufungua ukurasa mpya katika mahusiano yake na Afrika

Tangu mwanzo wa muhula wake, Rais wa Marekani Joe Biden alipendekeza kuwepo kwa ushirikiano wa karibu na Afrika ili kufunga ukurasa wa miaka ya Trump.

Naibu Waziri wa Biashara Don Graves mnamo Januari 8, 2021 mjini Wilmington.
Naibu Waziri wa Biashara Don Graves mnamo Januari 8, 2021 mjini Wilmington. AP - Susan Walsh
Matangazo ya kibiashara

Tangu kuwasili kwake katika Ikulu ya White, mckato wa kidiplomasia umeanza. Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alizuru bara hilo mnamo Novemba 2021.

Wiki iliyopita, Naibu Waziri wa Biashara Don Graves alitembelea Ivory Coast na Ghana na kuahidi ushirikiano zaidi na nchi hizo.

Katika kushawishi bara ambalo ni mara tatu ya ukubwa zaidi ya Marekani na ambalo linashikiliwa na mataifa yenye nguvu duniani, Washington inajua kwamba lazima itoe ushawishi wake. Baada ya Donald Trump kuitenga Afrika na dharau ya wazi aliyoonyesha, utawala wa Biden unaonyesha heshima zaidi kwa bara hili, ikisisitiza ushirikiano "bila malipo".

"Marekani imejitolea kuwa mshirika mmoja katika mchakato wa kuheshimiana, Don Graves, Naibu Waziri wa Biashara amebaini.

Miundombinu na malighafi

Hili lazima lieleweke kama nia iliyoelezwa ya Washington ya kujitofautisha na China, ambayo miradi yake mikubwa ya miundombinu inatumiwa na wafanyakazi wachache sana wa ndani na mara nyingi husababisha madeni makubwa kwa nchi za Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.