Pata taarifa kuu

Watu kadhaa wajeruhiwa katika shambulizi katika kituo cha treni New York

Watu kadhaa wamepigwa risasi na wengine kujeruhiwa Jumanne asubuhi katika kituo cha treni ya chini ya ardhi huko Brooklyn, New York, kulingana na idara ya zima moto ya jiji hilo.

Watu kadhaa walipigwa risasi katika kituo cha treni ya chini ya ardhi cha New York huko Brooklyn.
Watu kadhaa walipigwa risasi katika kituo cha treni ya chini ya ardhi cha New York huko Brooklyn. REUTERS - BRENDAN MCDERMID
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa idara ya Zima moto waliotumwa kwenye mtaa wa 36th katika kitongoji cha Sunset Park walikuta watu kadhaa wamepigwa risasi na vilipuzi, kulingana na msemaji wa Idara ya Zima moto huko New York.

Kwa mujibu wa chanzo cha polisi kinachofahamu upelelezi huo, taarifa za awali zinaeleza kuwa mtuhumiwa alikuwa amevaa nguo za kazi.

Takriban watu 13 wamejeruhiwa, kulingana na mamlaka.

Picha kutoka eneo la tukio wanaonekana abiria waliokuwa wametapakaa damu wakiwa wamelala kwenye sakafu ya kituo hicho.

Maelezo zaidi hayakupatikana mara moja.

Polisi wa jiji la New York imesema ilikuwa ikijibu ripoti za watu kujeruhiwa kwa risasi au mlipuko.

Treni zinazotoa huduma katika kituo hiki zilichelewa kwa saa moja za asubuhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.