Pata taarifa kuu
MAREKANI-USALAMA

Marekani: Watano wafariki, 40 wajeruhiwa kwenye gwaride la Krismasi Wisconsin

Takriban watu 5 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa siku ya Jumapili baada ya gari kupita kwenye vizuizi na kuingia kwenye gwaride la Krismasi katika mji wa Waukesha, Wisconsin, karibu na Milwaukee nchini Marekani. Polisi winasema "mtu mwenye maslahi" yuko kizuizini.

Wahudumu wa kutoka idara ya dharura wakikusanyika baada ya gari kupita kwenye Gwaride ya ya Krismasi, na kusababisha maafa na watu wengi wakijeruhiwa huko Waukesha, Wisconsin, Marekani Novemba 21, 2021.
Wahudumu wa kutoka idara ya dharura wakikusanyika baada ya gari kupita kwenye Gwaride ya ya Krismasi, na kusababisha maafa na watu wengi wakijeruhiwa huko Waukesha, Wisconsin, Marekani Novemba 21, 2021. © Scott Ash-USA TODAY NETWORK via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili huko Wisconsin, tukio la kufurahisha la bendi zilizoandamana na watoto wanaocheza dansi wakiwa wamevalia kofia za Santa liligeuka papo hapo na kuwa tukio la kusikitisha, wakati gari la aina ya SUV liliposambua vizuizi na kuwagonga watu wengi.

Tukio hilo lilisababisha vifo vya watu watano na wengine 40 kujeruhiwa, mamlaka imesema.

"Mtu mweye maslahi" yuko kizuizini, amesema Dan Thompson, Mkuu wa Polisi wa Waukesha, bila kuoa maelezo zaidi juu ya mtu binafsi au nia yake.

Tukio hilo lilirekodiwa moja kwa moja na kituo cha televiseni chajiji hilo na simu za rununu za wakaazi. Afisa wa polisi wa jiji alilifyatulia risasi gari hilo, akijaribu kulizuia.

Katika video moja, mtoto mdogo anaonekana akicheza dansi barabarani gari likipita kwa kasi, mita chache kutoka kwake, kabla ya kukimbilia kwa washiriki wa gwaride, umbali wa mita mia chache.

Kasisi wa Kikatoliki, waumini kadhaa na watoto wa shule ya Kikatoliki huko Waukesha ni miongoni mwa waliojeruhiwa, almesema Sandra Peterson, msemaji wa dayosisi ya Milwaukee.

Chris Germain, mmiliki mwenza wa studio Aspire Dance Center, anasema kulikuwa ntakriban watu 70 kwenye gwaride, wenye umri wa miaka 2 hadi 18, wakivutwa na mikokoteni. Bw Germain, ambaye binti yake mwenye umri wa miaka 3 alikuwa sehemu ya gwaride hilo, amesema alikuwa akiendesha gari mbele ya kundi lao alipoona gari la kahawia "lilikipita mbele yetu," afisa wa polisi alikuwa akimfuata.

Shahidi huyo anasema aliruka kutoka kwenye gari lake na kuwachukua wasichana waliokuwa nao na kuwafikisha mahali salama. 

”Kulikuwa na watoto wadogo wamelala barabarani, kulikuwa na maafisa wa polisi na wahudumu wa afya wakijaribu kuwashughulikia watu kadhaa waliokuwa sehemu ya gwaride hilo,” ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.