Pata taarifa kuu
MAREKANI-USALAMA

Wahamiaji nchini Marekani: Mexico yaomba msaada wa Washington

Serikali ya Marekani imeanza kuwarejesha makwao mamia ya wahamiaji, hasa raia wa Haiti, ambao walikuwa wamekusanyika katika kambi ya muda huko Texas katika siku za hivi karibuni.

Walinzi wa mpaka wa Marekani waliopanda farasi kujaribu kuwazuia wahamiaji wa Haiti kuingia kwenye kambi kwenye kingo za Rio Grande karibu na Daraja la Kimataifa la Acuna del Rio huko Del Rio, Texas Septemba 19, 2021.
Walinzi wa mpaka wa Marekani waliopanda farasi kujaribu kuwazuia wahamiaji wa Haiti kuingia kwenye kambi kwenye kingo za Rio Grande karibu na Daraja la Kimataifa la Acuna del Rio huko Del Rio, Texas Septemba 19, 2021. AFP - PAUL RATJE
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu, Septemba 20, Rais wa Mexico Andrés Manuel López Obrador alimsihi Joe Biden kushirikiana na Mexico na nchi za Amerika ya Kati ili kudhibiti uhamiaji badala ya watu kukamatwa na kufukuzwa kiholela bila kuzingatia sababu za kutoroka nchi zao.

Karibu wahamiaji 15,000, wengi wao raia kutoka Haiti walikuwa wamepewa hifadhi kwa siku kadhaa chini ya daraja huko Texas baada ya kuvuka mpaka kutoka Mexico.

Marekani imesema itatumia usafiri wa ndege kwa kufanikisha zoezi lake hilo.

Wahamiaji hawa waliwasili Del Rio, Texas, wakivuka Mto Rio Grande. Kutoka idadi iliyo chini ya 2,000 mwanzoni mwa juma lililopita, walikuwa zaidi ya 10,500 siku ya Ijumaa wiki iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa na meya wa mji huu wa mpakani, Bruno Lozano, ambaye anatarajia idadi kubwa ya wahamiaji kwa siku za karibuni kama hakuna hatua itakayochukuliwa.

Siku ya Jumamosi katika taarifa, Wizara ya Usalama wa Nchi ya Marekani ilisema "itapata ndege za ziada ili kuharakisha kasi na kuongeza uwezo wa kusafirisha wahamiaji hao kwa ndege kwenda Haiti na maeneo mengine" ndani kipindi cha saa 72 zijazo.

Picha za kuvutia za wahamiaji hawa waliokusanyika chini ya daraja wakati wa joto zimesababisha siku za hivi karibuni upinzani kutoka chama cha Republican lakini pia wabunge kadhaa na maseneta kutoka chama cha Democratic kumsihi Joe Biden atatue hali hiyo bila kuchelewa.

Mbali na machafuko ya kisiasa na ukosefu wa usalama ambao tayari ulikuwa umetanda huko Haiti, mnamo Agosti tetemeko baya la ardhi lilipiga kusini magharibi mwa nchi, na kuua zaidi ya wakaazi 2,200. Watu 650,000, ikiwa ni pamoja na watoto na vijana 260,000, wanaendelea kuhitaji "msaada wa dharura wa kibinadamu", kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.