Pata taarifa kuu
HAITI

Haiti: kura ya maoni ya katiba iliyopangwa kufanyika Juni 27 yaahirisha

Kura ya maoni ya katiba ambayo ilipingwa vikali,  haitafanyika Juni 27 nchini Haiti. Maafisa wa uchaguzi wametoa tangazo hilo Jumatatu jioni wiki hii, wakitoa sababu za kuongezeka kwa hivi karibuni kwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo. Kama hali ya kiafya inatia wasiwasi, kuna changamoto zingine zinazouia uchaguzi huo kufanyika.

Mmoja wa waandamanaji akishikilia Katiba ya Haiti wakati wa mkutano wa hadhara wa kutaka Rais Jovenel Moïse ajiuzulu, Februari 10, 2021 huko Port-au-Prince.
Mmoja wa waandamanaji akishikilia Katiba ya Haiti wakati wa mkutano wa hadhara wa kutaka Rais Jovenel Moïse ajiuzulu, Februari 10, 2021 huko Port-au-Prince. AP - Dieu Nalio Chery
Matangazo ya kibiashara

Ni vigumu kukusanya wafanyakazi wake na kuwaweka tayari katika kuandaa kura ya maoni kwa masharti ya kuheshimu sheria za usafi. Hivi ndivyo Tume Huru ya Uchauzi imethibitisha kuahirishwa kwa uchaguzi uliopangwa kufanyika Juni 27, huku ikibainisha kuwa ratiba mpya itapangwa kwa ushauri wa maafisa wa afya.

Kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wa COVID-19 ni ukweli nchini Haiti na hospitali chache ambazo zina uwezo wa kupokea wagonjwa waliowekwa karantini zimejaa watu. Haiti ilitangaza hali ya hatari tangu Mei 24.

Upinzani wataka kura ya maoni kufutwa

Sasa, ni dhahiri kwamba kura hii ya maoni ya katiba sio tena kisinizio kwa raia. Upinzani wa kisiasa na mashirika mengi ya kiraia yaliandamana mara kadhaa dhidi ya utaratibu huo wa kufanyika kwa kura ya maoni ya Katiba, ambayo wanaona kuwa ni kinyume cha sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.