Pata taarifa kuu
MAREKANI

Marekani: Joe Biden kutetea mipango yake ya matumizi mbele ya Bunge la Congress

Rais wa Marekai Joe Biden anatarajiwa kufichua mpango mpya wa dola  Bilioni 1.8 (sawa na euro Bilioni 1.491) kwa familia na elimu Jumatano katika hotuba yake ya kwanza kwa Bunge, maafisa wa White House wamesema.

Joe Biden pia atawataka wabunge kupitisha sheria inayolenga kupunguza ghasia za polisi, maafisa katika utawala wake wamesema.
Joe Biden pia atawataka wabunge kupitisha sheria inayolenga kupunguza ghasia za polisi, maafisa katika utawala wake wamesema. JIM WATSON AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa kutoka chama cha Democratic, ambaye anasisitiza juu ya umuhimu wa kuwekeza kwa Markani ili kukidhi ushindani kutoka China, anatarajia  kutumia fursa ya hotuba hii kuthibitisha kuwa mpango huu mpya na mradi wa maendeleo ya miundombinu ya zaidi ya dola Bilioni 2,000 ambao ulifichuliwa hivi karibuni, ni jumla ya takriban dola Bilioni 4, ni muhimu kwa mustakabali wa Marekani.

Joe Biden pia atawataka wabunge kupitisha sheria inayolenga kupunguza ghasia za polisi, maafisa katika utawala wake wamesema. Makamu wa rais wa zamani wa Barack Obama atarejelea katika hafla hii kwa mauaji ya mara kwa mara ya Wamarekani weusi wanaouawa na maafisa wa polisi na shutuma za ubaguzi wa kimfumo ndani ya polisi, na kukaribisha kazi inayofanywa na maafisa wengi wa polisi.

Mpango mpya wa Joe Biden, ambao utafichuliwa kwa kina Jumatano, unajumuisha dola Bilioni 1,000 katika matumizi mapya kwa miaka kumi kwa elimu na utunzaji wa watoto na dola Bilioni 800 bilioni kwa mikopo ya ushuru kwa familia zenye kipato cha kati na dhaifu, kulingana na maafisa wa Ikulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.