Pata taarifa kuu
MAREKANI

Biden amuagiza Harris kufanya kazi na Mexico kuhusu suala la wahamiaji

Rais wa Marekani amemtaja Makamu wake Kamala Harris, kuongoza harakati za kupata suluhu ya kuendelea kushuhudiwa kwa wimbi kubwa ya wahamiaji hasa watoto wanaoingia nchini humo kutokea katika mpaka wa Mexico.

Rais wa Marekani Joe Biden akiambatana na Makamu wake Kamala Harris wakati anaongea na Katibu wa HHS Xavier Becerra katika mkutano na washauri wa masuala ya uhamiaji katika chumba cha kulia cha Ikulu ya White House, Washington, Marekani, Machi 24, 2021.
Rais wa Marekani Joe Biden akiambatana na Makamu wake Kamala Harris wakati anaongea na Katibu wa HHS Xavier Becerra katika mkutano na washauri wa masuala ya uhamiaji katika chumba cha kulia cha Ikulu ya White House, Washington, Marekani, Machi 24, 2021. REUTERS - JONATHAN ERNST
Matangazo ya kibiashara

Biden amesema ana uhakika makamu wake atasaidia kupata suluhu ya changamoto hiyo kwa kuongoza mazungumzo na mataifa jirani, wakati huu serikali yake ikikosolewa kwa namna inavyoshughulikia kuwasili kwa wahamiaji nchini humo.

Hatua hiyo inakuja wakati utawala wa Marekani unapambana kudhibiti idadi kubwa ya wwahamiaji kwenye mpaka na Mexico, matatizo ambayo rais wa Joe Biden amelaumu sera za "kibabe" za mtangulizi wake wa Donald Trump kutoka chama cha Republican.

Marekani itahitaji msaada kutoka Mexico na nchi zinazounda pembetatu kaskazini mwa Amerika ya Kati - Honduras, Guatemala na El Salvador - amesema Joe Biden, na kuongeza kuwa Kamala Harris "amekubali kuongoza juhudi zetu za kidiplomasia na kufanya kazi na nchi hizi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.