Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFGANISTAN

Utawala wa Biden kutathmini upya mkataba na Taliban

Marekani itafikiria kujadili upya mtataba uliofikiwa mwaka jana kati ya utawala wa Donald Trump na kundi la Taliban kutoka Afghanistan, Ikulu ya White House imesema.

Wapiganaji wa Taliban
Wapiganaji wa Taliban Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mshauri mpya wa usalama wa kitaifa wa Marekani, Jake Sullivan, amemfahamisha mwenzake wa Afghanistan katika mazungumzo ya simu, White House imsbaii katika taarifa yake.

Baada ya mazungumzo ya zaidi ya mwaka mzima, Marekani ilisaini makubaliano ya kihistoria na kundi la Taliban, yanayosafisha njia kwa Marekani kuondoa wanajeshi wake nchini Afghanistan. Makubaliano hayo yalisainiwa mjini Doha, Qatar, Februari 29.

Pande zote mbili, Marekani na Wataliban, zilisifu hatua hiyo iliyopigwa zikiitaja kuwa ya kihistoria, na ambayo itasaidia kurejesha amani baada ya miaka mingi ya vita nchini Afghanistan.

Kutiwa saini mkataba huo kulitimiza moja ya ahadi muhimu ya wakati wa uchaguzi iliyotolewa na rais Donald Trump ya kuindoa Marekani kutoka vita visivyokwisha ikiwemo nchini Afghanistan.

 

Wakati huo Umoja wa Ulaya ulisema unaunga mkono hatua ya kufikiwa makubaliano hayo baina ya Marekani na Wataliban, lakini ikahimiza kuendelea kuheshimiwa kwa haki za binadamu na za wanawake nchini Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.