Pata taarifa kuu
MEXICO

Mexico yatoa hifadhi ya kisiasa kwa Julian Assange

Kufuatia tangazo la Mahakama ya Uingereza kutomsafirisha Julian Assange kwenda MArekani, Rais wa Mexico Andrés Manuel López Obrador ametoa wito kwa mwanzilishi wa mtando wa kiuchunguzi wa  WikiLeaks kwa kumpa hifadhi ya kisiasa.

Julian Assange
Julian Assange REUTERS/John Stillwell
Matangazo ya kibiashara

Mexico itahakikisha usalama wake unalindwa vilivyo na kumpa haki ya ukimbizi. Julian Assange hataingilia masuala ya kisiasa ya nchi yoyote. Lakini vyombo vya wa habari nchini Mexico vinaona hatua hii ya rais wa Mexico kama hoja tatanishi kwa njia nyingi.

Rais López Obrador alitoa pendekezo lake hilo Jumatatu, Januari 4, wakati vyombo vya habari nchini Mexico winamchukulia Julian Assange kama mkimbizi mkubwa. Ikiwa Mexico itatoa hifadhi ya ukimbizi kwa mwanzilishi wa WikiLeaks, uhusiano na serikali ya baadaye ya Joe Biden unaweza kuvunjika mapema.

Lakini López Obrador, anadai kutetea utamaduni wa kuwapokea wakimbizi wa kisiasa ulioanzishwa miaka mingi na Mexico. Amesema anataka kumlinda mwanahabari aliyeathiriwa na mfumo wa kimabavu. Na amesema Mahakama ya Uingereza kukataa kumsafirisha Julian Assange nchini Marekani ni "ushindi wa haki."

Taarifa za WikiLeaks zilizovuja zilionyesha kuwa, mapema mwaka 2006, Washington haikufurahia umaarufu wa López Obrador na nafasi yake kuwa siku moja ataingia madarakani.

Assange mwenye umri wa miaka 49 anatakiwa nchini Marekani baada ya mwaka 2010 na 2011 kuchapisha maelfu ya taarifa za siri za Marekani katika matandao wake, hatua ambayo Marekani inasema ilikuwa kinyume cha sheria na kuhatarisha usalama wa watu.

Baada ya uamuzi huu, Marekani ina siku 14 kukataa rufaa. Assange mwenyewe amekuwa akisema mashtaka dhidi yake nchini Marekani, yamechochewa kisiasa.

Assange ambaye amekuwa nchini Uingereza tangu mwaka 2012 na wakati mmoja kupewa hifadhi katika ubalozi wa Ecuador, alikuwa Mahakamani na wakati Jaji akisoma uamuzi dhidi yake, alionekana akifumba macho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.