Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Trump amtuhumu Biden kwa kujaribu 'kuiba' uchaguzi, zoezi la uhesabuji laendelea

Rais wa Marekani Donald Trump amemshtumu mpinzani wake wa kutoka chama cha Democratic Joe Biden kwa kujaribu "kuiba" uchaguzi, bila ushahidi wowote thabiti, wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea, huku kura zikikaribiana kwa wawili hao.

Watu wakitazama usiku wa uchaguzi kwenye televiseni kubwa iliyowekwa ukutani karibu na ikulu ya White House huko Washington, Novemba 3, 2020.
Watu wakitazama usiku wa uchaguzi kwenye televiseni kubwa iliyowekwa ukutani karibu na ikulu ya White House huko Washington, Novemba 3, 2020. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Tuko mbele na mbali, lakini wanajaribu kuiba uchaguzi. Hatutawaacha wafanye hivyo", Donald Trump ameandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter,.

Wakati huo huo mtandao wa Twitter umeonya watumiaji wake, ukibaini kwamba ujumbe huo ni wa "kupotosha".

Katika hotuba fupi kutoka ngome yake ya Wilmington, Delaware, Joe Biden amesema yuko kwenye 'nafasi nzuri' ya kushinda.

"Muwe na imani, tutashinda!" , amesema makamu wa zamani wa Barack Obama mbele ya wafuasi wake waliokusanyika katika kumsikiliza.

"Tuna imani ya kushinda katika jimbo la Arizona," jimbo muhimu, ameongeza Joe Biden, mwenye umri wa miaka 77, akitoa wito kwa uvumilivu wakati kunaripotiwa mkanganyiko kuhusu matokeo katika majimbo kadhaa muhimu.

Katika Marekani iliyokumbwa na migogoro ya kiafya, kiuchumi na kijamii kwa kiwango kikubwa cha kihistoria, Wamarekani wameendelea wakijiandaa kwa usiku mrefu, hata kwa siku nyingi za kusubiri, baada ya kampeni zilizokuwa ni zenye kushambuliana.

Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa Biden ameshinda kwenye majimbo ya Virginia, Delaware,Vermont Connecticut, Illinois, Maryland, Massachusetts, New Jersey na Rhode Island huku Trump akiyanyakua majimbo la Virginia magharibi, Kentucky, na South Carolina, Alabama, Mississippi, Oklahoma na Tennessee.

Mpaka sasa Joe Biden anaongoza kwa kura za wajumbe maalum 131 na Trump akiwa na idadi ya kura 98 za wajumbe maalum. Matokeo yanaendelea kutangazwa.

Katika Jimbo la Florida rais anaye maliza muda wake Donald Trump anaongoza kwa karibu kura zote zilizohesabiwa.

Trump anaelekea kupata faida kwa wapiga kura wenye miaka 65 na zaidi kwa (51% kwa 48%).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.