Pata taarifa kuu
UN-MAREKANI-USALAMA

Mkataba wa kupiga marufuku silaha za nyuklia kuanza kutumika

Mkataba wa kimataifa wa kupiga marufuku silaha za nyuklia umeidhinishwa na nchi 50 na utaanza kutumika katika muda wa siku 90. wakati huo huo Guterres amesema mkataba huu unawakilisha hatua ya kujitolea inayolenga kuondolewa kabisa silaha za nyuklia, jambo ambalo linapewa kipaumbele na Umoja wa Mataifa.

Wanaharakati wa kampeni ya Kimataifa wanatetea kutokomezwa dhidi ya silaha za Nyuklia (ICAN) wakijifananisha kama Donald Trump na Kim Jong-un wakiwa nje ya ubalozi wa Korea Kaskazini huko Berlin Septemba 13.
Wanaharakati wa kampeni ya Kimataifa wanatetea kutokomezwa dhidi ya silaha za Nyuklia (ICAN) wakijifananisha kama Donald Trump na Kim Jong-un wakiwa nje ya ubalozi wa Korea Kaskazini huko Berlin Septemba 13. Britta Pedersen / dpa / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema mkataba huo utakaoanza kutekelezwa Januari 22 mwakani ni kilele cha harakati za ulimwenguni kote za kuwakumbusha watu juu ya matokeo mabaya kwa binadamu kutokana na matumizi ya silaha za nyuklia na pia ni harakati za kuwakumbuka watu walioathiriwa na milipuko ya nyuklia ikiwa ni pamoja na athari za majaribio ya silaha hizo, ambapo wengi wao ni miongoni mwa walioutetea mkataba huu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezipongeza nchi 50 zilizoidhinisha mkataba huo na amesifu kazi muhimu iliyofanywa na asasi za kiraia katika kuandaa mazungumzo na kuhakikisha makubaliano yaliyofikiwa, amesema msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric.

Hata hivyo wanaharakati wanaopinga matumizi ya nyuklia wameisifu hatua hiyo lakini Marekani na mataifa mengine yenye nguvu yanayomiliki nyuklia wameupinga vikali mkataba huo.

Marekani imebaini kwamba mkataba huo wa kupiga marufuku silaha za yyuklia, unaojulikana kama TPNW, unarudisha nyuma juhudi za upokonyaji wa silaha hizo na pia ni wa hatari.

Kulingana na vyanzo rasmi, Marekani imeyaandikia mataifa yaliotia saini mkataba huo na kusema serikali yake inaamini kuwa yalifanya ''kosa la kimkakati'' na imeyahimiza kubatilisha misimamo yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.