Pata taarifa kuu
UN-USALAMA-SIASA-USHIRIKIANO

Umoja wa Mataifa waadhimisha kumbukumbu ya miaka 75 katika hali ya mivutano

Viongozi wa dunia wamehotubia Umoja wa Mataifa katika mkutano kupitia njia ya video kuadhimisha miaka 75 tangu kuundwa kwa Umoja huo baada ya vita vya pili vya dunia.

Makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Septemba 21, 2020.
Makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Septemba 21, 2020. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Maadhimisho hayo hayajawakutanisha viongoizi hao kwa sababu ya janga la Corona ambalo limewaathiri Mamilioni ya watu duniani.

Rais wa China Xi Jinping amesema Umoja wa Mataifa unadhimisha miaka 75, na hakuna taifa linastahili kudhibiti masuala ya dunia, ukiwa ni ujumbe kwa Marekani.

Katibu Mkuu wa umoja huo Antinio Guteress, naye ameelezea mafanikio na changamoto za Umoja huo kwa muda wa miaka 75.

Baada ya hotuba fupi ya kufungua mkutano huo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Rais wa Brazil Jair Bolsonaro atapewa nafasi ya kwanza kuhutubia mkutano huo, kama ada, akifuatiwa na rais wa Matekani Donald Trump. Mada zitakazojadiliwa kando ya mkutano huo ni pamoja na janga hatari la Covid-19, hali ya hewa, Lebanon, Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.