Pata taarifa kuu
ARGENTINA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Masharti yarejeshwa nchini Argentina licha ya kuongezeka kwa visa vya maambukizi

Argentina imeendelea kurekodi visa vipya vya maambukizi ya virusi vya Corona tangu Ijumaa wiki hii, wakati serikali ikitangaza kulegeza hatua za kukabiliana na maambukizi ya janga hilo nchini nzima.

Katika mji mkuu Buenos Aires, mamlaka zimetangaza kwamba zitaruhusu mikahawa kuanza kuhudumia wateja wao.
Katika mji mkuu Buenos Aires, mamlaka zimetangaza kwamba zitaruhusu mikahawa kuanza kuhudumia wateja wao. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hatimaye serikali imeruhusu mikusanyiko hadi watu kumi katika maeneo ya umma kwa sharti la kuvaa barakoa.

Kulingana na takwimu rasmi, kesi mpya 11,717 za maambukizi ya virusi vya Corona zimethibitishwa katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, kwa jumla ya kesi 392,009 za maambukizi ikijumuishwa vifo vya watu 8,271.

Serikali iliweka masharti ya kiafya Machi 20 ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona. Hatua zilizochukuliwa za kulegeza masharti zitatumika hadi Septemba 20, Rais Alberto Fernandez amesema katika kenye televisheni.

Katika mji mkuu Buenos Aires, mamlaka zimetangaza kwamba zitaruhusu mikahawa kuanza kuhudumia wateja wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.