Pata taarifa kuu
BRAZILI-BOLSONARO-HAKI

Brazil: Bolsonaro akabiliwa na uchunguzi, hatua ya kwanza kuelekea kujiuzulu

Rais wa Brazil Jair Bolsonaro anaweza kukabiliwa na mashtaka kufuatia kuanzishwa kwa uchunguzi baada ya mahakama ya juu nchini humo kuagiza uchunguzi kuhusu madai ya "kuingilia" katika kesi za mahakama, madai yalitolewa na waziri wake wa zamani wa Sheria.

Rais wa Brazil Jair Bolsonaro anashtumiwa na Waziri wake wa zamani wa Sheria Sergio Moro kuingilia kazi za mahakama.
Rais wa Brazil Jair Bolsonaro anashtumiwa na Waziri wake wa zamani wa Sheria Sergio Moro kuingilia kazi za mahakama. EVARISTO SA, Sergio LIMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jaji wa Mahakama Kuu ya Brazil Celso de Mello ameipa polisi muda wa siku 60 kumhoji Sergio Moro, Waziri wa zamani wa Sheria na bingwa wa kupambana na ufisadi ambaye alijiuzulu kwenye nafasi yake siku ya Ijumaa, kulingana na uamuzi ambao shirika la habari la AFP limepata kopi.

Uchunguzi kama huo unaweza kufungua njia kwa utaratibu wa kutimuliwa madarakani dhidi ya Jair Bolsonaro, au kwa mashtaka dhidi ya Sergio Moro kwa makosa ya ushahidi wa uwongo.

Waziri huyu wa zamani maarufu nchini Brazili, maarufu kwa operesheni yake ya kupambana na ufisadi "Lava Jato" (kuosha haraka), alikabidhi barua yake ya kujiuzulu siku ya Ijumaa baada ya mkuu wa polisi nchini humo kufukuzwa kazi. Polisi nchini Brazili iko chini ya mamlaka ya Wizara ya Sheria.

"Kupinduliwa kwa mkuu wa Polisi bila sababu halisi ni kuingilia kisiasa Wizara ya Sheria, uamuzi ambao unaangusha sifa yangu na ile ya serikali," Sergio Moro alisema siku ya Ijumaa.

"Rais aliniambia kuwa anataka kumteua mtu ambaye ana mawasiliano naye kibinafsi, ambaye atakuwa akimwita ili kupata taarifa kuhusu uchunguzi," aliongezea wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Brasilia.

Rais kwa upande wake alithibitisha hadharani siku ya Ijumaa kwamba madaia hayo hayana "msingi" wowote na kuongeza kuwa waziri wake wa zamani alikuwa akijihusisha "na mambo yake" binafsi, hasa kuwa na "kiti katika Mahakama Kuu".

Kulingana na jaji de Mello, makosa yanayodaiwa dhidi ya rais yanaonekana kuwa na "uhusiano wa karibu na majukumu ya rais", ambayo yanaomba kwanza aondolewe kinga.

Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Brazili unaonyesha makosa saba ambayo Bwana Bolsonaro anaweza kuwa alifanya, ikiwa ni pamoja na kutumia madaraka vibaya na kuzuia shughuli ya mahakama.

Baada ya kujiuzulu, Bw. Moro alionesha kwenye runinga mazungumzo yake na rais Bolsonaro kupitia WhatsApp ambapo rais huyo akimshinikiza amfute kazi mkuu wa Polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.