Pata taarifa kuu
MAREKANI-SANAA-HAKI

Hukumu dhidi ya mcheshi nguli Bill Cosby yazua mjadala Marekani

Mwigizaji maarufu na mkongwe nchini Marekani, Bill Cosby amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu hadi kumi jela, baada ya mahakama kumkuta na hatia ya kuwadhalilisha kingono wanawake zaidi 60 miaka 14 iliyopita.

Mcheshi nguli na mwigizaji maarufu Bill Cosby, ahukumiwa kifungo cha miaka 3 hadi 10 kwa kosa la unyanyasaji wa kimapenzi, Septemba 25, 2018.
Mcheshi nguli na mwigizaji maarufu Bill Cosby, ahukumiwa kifungo cha miaka 3 hadi 10 kwa kosa la unyanyasaji wa kimapenzi, Septemba 25, 2018. Courtesy Montgomery County Correctional Facility/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Cosby aliyekuwa akikabiliwa na mashitaka kadha yaliyotokana na madai ya wanawake wengi alikutwa na hatia mwezi Aprili mwaka huu katika makosa matatu ya udhalilishaji wa kingono kwa kumpa dawa na kumfanyia tendo la ngono Andrea Constand mwaka 2004.

Cosby mwenye umri wa miaka 81, alikuwa akitajwa na mashabiki wake kama baba wa Marekani na hukumu yake imeleta mgawanyiko wa mawazo, baadhi wakienda mbali zaidi na kuingiza dhana ya ubaguzi wa rangi.

Cosby kwa mara ya kwanza alikutwa na hatia mwezi April mwaka huu na siku ya Jumanne wiki hii baraza la wazee wa mahakama kwa kauli moja waliridhia kumtia hatiani Cosby na kumuhukumu kifungo jela.

Mawakili watetezi wa Cosby, mwenye umri wa miaka 81, walionyesha dalili awali kuwa watakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.