Pata taarifa kuu
UFARANSA-UN-USALAMA

Emmanuel Macron: Ubabe hauleti suluhu bali unaongeza machafuko

Mkutano Mkuu wa 73 wa Umoja wa Mataifa ambao ulianza tangu Jumanne wiki hii huko New York nchini Marekani umeendelea kugubikwa na mvutano na hotuba za kushtumiana kati ya baadhi ya viongozi wa nchi.

Kwenye jukwaa la Umoja wa Mataifa, Emmanuel Macron aomba ushirikiano wa kikanda na wa kimataifa Septemba 25, 2018.
Kwenye jukwaa la Umoja wa Mataifa, Emmanuel Macron aomba ushirikiano wa kikanda na wa kimataifa Septemba 25, 2018. REUTERS/Carlo Allegri
Matangazo ya kibiashara

Baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, Rais Donald Trump na Emmanuel Macron kila mmoja alipewa nafasi ya kutoa hotuba yake.

Rais wa Marekani alitumia fursa katika Mkutano huo Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa kushambulia kwa maneno makali serikali ya Iran. "Viongozi wa Iran wanachochea vurugu na uharibifu mkubwa," alianza akisema Donald Trump. "Udikteta huu wa kutumia fedha kwa kutengeneza makombora ya nyuklia, kuendelea ukandamizaji wa ndani, kudhamini ugaidi, kufanya uharibifuna mauaji huko Syria na Yemen. Marekani ilizindua kampeni ya shinikizo la kiuchumi ili kuzuia feha zinazohitajika kwa serikali kwa mipango yake ya mauaji, "Rais wa Marekani amesema baada ya kurejesha mnamo mwezi Mei vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran.

Miezi michache baada ya Matekani kujitoa kwenye mkataba wa nyuklia, Rais wa Marekani amezitaka nchi nyingine kuchukua hatua kama hiyo: "Serikali ambayo kauli yake mbiu ni" Kuiona Marekani imeangamia"na kuitishia Israeli kwamba itageuzwa jivu mara moja, haiwezi kuwa na nia njema ya kusitisha mpango wake wa nyuklia. Haiwezekani. Tunatoa wito kwanchi zote ulimwenguni kutenga utawala wa Iran wakati ambapo itakuwa bado na mpango wake wa kuendeleza ukandamizaji wake. "

Kwa upande wake, Rais wa Iran, Hassan Rohani amesema hashangazwi na msimamo wa Donald Trump, ambaye amezitaka nchi zote duniani kuitenga Iran. Hassan Rohani ameishtumu Marekani kutaka "kuupindua" utawala wa Tehran. "Ni jambo linalojulikana kuwa Marekani inaonesha wazi mpango wake unaolenga kupindua serikali ya Iran, na ndio maana imeendelea kusisitiza kuhusu mazungumzo," amesema Rais Rohani ambaye ameielezea msimamo wa Marekani kuwa ni "ugaidi wa kiuchumi" na kusema kurejeshwa kwa vikwazo vya Marekani ni "ukiukwaji wa haki kwa maendeleo".

Hassan Rohani amefutilia mbali wazo lolote la mazungumzo kati ya nchi yake na Marekani. Hassan Rohani,hata hivyo, amesema kuwa mazungumzo yanaweza kuendelea katika Umoja wa Mataifa.

Wakati huo huo Raisa aw Ufaransa Emmanuel Macron ameomba Jumuiya ya kimataifa kuingilia kati kuhusu mvutano kati ya Iran na Marekani

Rais Macron ameomba kuwepo na mshikamano, ushirikiano na mazungumzo ili kukabiliana na changamoto na hasa mgogoro wa Iran.

Emmanuel Macron amesema katika Umoja wa Mataifa kuna kile alichoeleza ukosefu wa usawa ambao ulianzishwa baada ya miaka ya 1945. Rais Macron amebaini kwamba kutokwepo na usawa katika Umoja w Mataifa ndio chanzo cha matatizo ya sasa. Rais wa Ufaransa amejaribu kupendekeza ufumbuzi wake ili kuboresha hali hiyo.

Amesisitiza kuhusu heshima kwa uhuru wa wawanchi, kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kuboresha dhamana za kimataifa. Emmanuel Macron amerejelea kauli yake kwamba haamini kuwa "ubabe unaweza kuleta suluhu na kuendeleza dunia hii, lakini iwapo kutaanzishwa sheria za pamoja, mambo yanaweza kuwa sawa", huku akizitaja nchi zinazokabiliwa na migogoro - Syria, Libya, Israel na Palestina, akionyesha kwamba ubabe haujazaa matunda mpaka sasa na kinyume chake kumeongezeka machafuko na uhasama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.