Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-VIKWAZO

Marekani yaweka vikwazo vipya dhidi ya Urusi

Marekani imewawekea vikwazo vipya maafisa wa Urusi, ikiwa ni pamoja na vigogo na viongozi wa serikali walio karibu na rais wa nchi hiyo Vladimir Putin, na makampuni na mashirika 14 kwa "shughuli hasidi" za Moscow zinazolenga kuhatarisha demokrasia ya nchi za Magharibi, Waziri wa Fedha Steve Mnuchin amesema.

Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, mjini Hamburg, Julai 7, 2017.
Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, mjini Hamburg, Julai 7, 2017. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Hatua hizi zimezochukuliwa chini ya sheria "Dhidi ya madui wa Marekani" (CAATSA) zinazolenga kuadhibu Urusi kwa kuunganisha Crimea katika aridhi yake mnamo mwaka 2014, ushiriki wake katika vita vya Syria na kuingilia katika uchaguzi wa urais wa Marekani wa mwaka 2016.

Mnamo Machi 15, Washington tayari iliwawekea vikwazo watu 19 na taasisi tano, ikiwa ni pamoja na idara ya ujasusi ya Urusi.

Kwa upande wake Konstantin Kosachev, mwenyekiti wa kamati ya masuala ya kimataifa ya Halmashauri ya Shirikisho, taasisi ya juu ya Bunge, amelaani visivyokua na "msingi na vyenye uadui ", shirika la habari la Interfax limearifu.

Miongoni mwa wale waliolengwa na vikwazo vipya vya Marekani, ni pamoja na maafisa walio karibu na Vladimir Putin, Oleg Deripaska, mwanachama wa Halmashauri ya Shirikisho Suleiman Kerimov, ambaye familia yake inasimamia kampuni ya Polyus, Alexey Miller, Mkurugenzi Mkuu wa Gazprom, na katibu wa Baraza la Usalama la Kitaifa, Nikolai Patrushev.

Makampuni yaliyowekewa vikwazo ni pamoja namakampuni ya EN, yanayosimamiwa na Oleg Deripaska, na kampuni ya Renova ya Viktor Vekselberg, pamoja na kampuni ndogo ya Gazprom.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.