Pata taarifa kuu
MAREKANI-YOU TUBE-USALAMA

Milio ya risasi yasikika kwenye makao makuu ya YouTube

Mwanamke mmoja aliwajeruhi kwa risasi watu watatu, ambapo mmoja yuko katika hali mbaya. Tukio hilo lilitokea siku ya Jumanne kwenye makao makuu ya YouTube karibu na mji wa San Francisco, nchini Marekani na kusababisha hofu miongoni mwa wafanyakazi.

San Bruno, California, Aprili 3, 2018. Polisi wanakwenda kwenye majengo ya YouTube ambako milio ya risasi ilisikika.
San Bruno, California, Aprili 3, 2018. Polisi wanakwenda kwenye majengo ya YouTube ambako milio ya risasi ilisikika. Justin Sullivan/Getty Images/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama mshambuliaji alijiua baada ya kisa hicho.

Polisi inasema shambulio hilo linahusiana na mgogoro wa kibinafsi lakini vyombo vya habari vimetoa maelezo tofauti kuhusu wasifu wa mshambuliaji huyo.

Kwa mujibu wa gazeti la San Francisco Chronicle, mtuhumiwa, anayetambuliwa kama mwanamke kutoka kusini mwa California, alikuwa na chuki dhidi ya YouTube, akiishutumu kwenye tovuti yake kutorusha video zake, ambapo baadhi ya video hizo zinaonyesha wanyama wakiteswa. Kwa mujibu wa gazeti la Mercury News, baba wa mwanamke huyo amethibitisha kwamba mwanae alikua na chuki dhidi ya You Tube.

Kwa mujibu wa polisi, ambayo haikutaja jina lolote, mwanamke mmoja aliwapiga risasi watu kwenye makao makuu ya YouTube wakati wa chakula cha mchana, kabla ya kujiua kwa bunduki yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.