Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-TRUMP

Trump azuia kuchapishwa kwa nyaraka kuhusu madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi wa Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump amezuia kuchapishwa kwa nyaraka iliyoandaliwa na wabunge wa Democratic kuhusu madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2016.

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya Marekani imesema, nyaraka hiyo haiwezi kuwekwa wazi kwa sababu, kuna taarifa za siri ambazo hazistahili kufahamika kwa umma kwa sababu mbalimbali.

Nyaraka hii, ilitarajiwa kupinga ile ya awali iliyotolewa na wabunge wa Republican, ikionesha kuwa wachunguzi wa FBI walikuwa wanamwonea rais Trump kuhusu ushirikiano wake na Urusi wakati wa Uchaguzi huo.

Kiongozi wa wabunge wa Democratic Nancy Pelosi amesema hatua ya rais Trump ni kuzuia ukweli kuhusu kilichotokea.

Urusi imeendelea kusema haikumsaidia Trump kushinda Uchaguzi huo.

Shirika la FBI linaendelea kuchunguza madai kuwa Urusi ilimsaidia Trump kushinda Uchaguzi wa urais, lakini Trump anakanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.