Pata taarifa kuu
MAREKANI

Maelfu waandamana Boston kudai uhuru wa kujieleza

Maelfu ya waandamanaji wanaopinga ubaguzi wa rangi jana Jumamosi walifurika katika jiji la Boston nchini Marekani na kukusanya wananchi wa rangi nyeupe na kusababisha mvutano na polisi ingawa waliepuka vurugu kubwa ambazo ziliharibu tukio kama hilo mapema wiki hii huko Virginia.

Maelfu ya waandamanaji wanaopinga ubaguzi wa rangi wakiandamana mjini  Boston
Maelfu ya waandamanaji wanaopinga ubaguzi wa rangi wakiandamana mjini Boston REUTERS/Stephanie Keith
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yalliyojulikana kama uhuru wa kujieleza ya makundi ya mrengo wa kulia yalipangwa kufanyika hadi jioni lakini nusu saa kabla ya wakati huo polisi waliwasindikiza washiriki wake ambao idadi yao ilionekana kuwa kubwa ili kulinda usalama.

Rais wa Marekani Donald Trump aliandika katika ukurasa wake wa twitter kuwa anaunga mkono maandamano hayo na uhuru wa kujieleza.

Maandamano kama hayo yalifanyika huko Virginia mapema juma hili na kusababisha vurugu zilizoshutumiwa vikali na rais Trump.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.