Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-UBAGUZI

Trump alaani makundi yanayochochea chuki katika mji wa Charlottesville

Rais wa Marekani Donald Trump hatimaye amelaani "vurugu ya ubaguzi wa rangi" zilizosababisha kifo cha mtu mmoja na ishirini kujeruhiwa katika mji wa Charlottesville.

Donald Trump aongelea Agosti 14, 2017, kutoka White House kuhusu vurugu zinazotokana na ubaguzi wa rangi katika eneo la Charlottesville, Marekani.
Donald Trump aongelea Agosti 14, 2017, kutoka White House kuhusu vurugu zinazotokana na ubaguzi wa rangi katika eneo la Charlottesville, Marekani. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Pamoja na vurugu zilizotokea wakatu wa maandamano yaliyopigwa marufuku ya wafuasi wa Kinazi na wazungu wenye itikadi kali za ubaguzi wa rangi, Donald Trump aliharakia kulaani machafuko hayo yaliyotokana na "makundi mengi," bila hata hivyo kufafanua.

Katika majibu yake ya kwanza kuhusu vurugu zilizotokea katika mji wa Charlottesville, hasa kwenye Twitter, Donald Trump aliyashtumu makundi ya mrengo wa kulia dhidi ya waandamanaji. Kauli ambayo ilizua hali ya sintofahamu nchini Marekani, ambapo inafahamika kwamba mfuasi anayepinga itikadi za Kifashistindio aliuawa na mtu aliye karibu kundi lenye itikadi za Kinazi.

Ilichukua karibu saa 48 kwa Donald Trump kurekebisha baada ya kauli yake iliyozua utata siku ya Jumamosi, 12 Agosti. siku ya Jumatatu, rais wa Marekani hatimaye ilitumia maneno yaliyosubiriwa awali, huku akilitaja kundi la Ku Klux kama watu wa itikadi za Kifashisti, wale wenye itikadi za Kinazis, watu wenye itikadi za ubaguzi wanaosambaza kauli mbovu za kuchochea chuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.