Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-HAKI

Amri mpya ya Trump kuhusu wahamiaji yapata pigo mahakama yazuia

Majaji nchini Marekani wamepinga kwa mara nyingine tena sheria mpya ya uhamiaji piga marufuku raia wa kigeni kutoka baadhi ya nchi, za Kiislamu kuingia nchini Marekani.

Donald Trump, Machi 15, 2017.
Donald Trump, Machi 15, 2017. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo wa majaji umekuja ikiwa ni saa chache kabla ya sheria hiyo kuanza kutumika rasmi.

Hakimu katika jimbo la Hawaii akishirikiana na wanasheria wa serikali wamesema sheria hiyo mpya ya Donald Trump itawanyima haki waislam wa Marekani sambamba na wahamiaji.

Trump amesema kuwa uamuzi huo wa makahama ni la kushangaza na sio haki. Hata hivyo Wanasheria wa serikali wame panga kuipeleka kesi hiyo katika mahakama za juu zaidi.

Hili ni pigo jingine kwa Donald Trump wakati ambapo sheria hiyo ingeanza kutumika Alhamisi hii, Machi 16, 2017. Sheria hii ilikua inalenga kuwazuia kwa kipindi cha miezi mitatu raia kutoka mataifa sita ya Kiislamu nchini Marekani.

Nchi sita hizo ni pamoja na Libya, Somalia, Sudan, Yemen, Syria na Iran. Kutokana na uamuzi huo wa majaji sheria hiyo haitoanza kutumika Alhamisi hii kama ilivyokua imepangwa.

Donald Trump amesema uamuzi wa majaji hauna maana, na kubaini kwamba atapambana hadi mwisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.