Pata taarifa kuu
MAREKANI-JAMII

Mashirika yasio ya kiserikali yaalani agizo rasmi la Trump

Mashirika ambayo yanaunga mkono utoaji mimba na kutoa huduma za afya ya uzazi barani Afrika wamelaani uamuzi wa Donald Trump kukomesha ufadhili kwa mashirika yaotoaji Mimba nchini Marekani.

Rais mpya wa marekani alisaini agizo rasmi la rais linaofuta ufadhili na fedha za mashirika ya kimataifa yasio ya kiserikali zinazotumiwa kwa kutoa mimba.
Rais mpya wa marekani alisaini agizo rasmi la rais linaofuta ufadhili na fedha za mashirika ya kimataifa yasio ya kiserikali zinazotumiwa kwa kutoa mimba. AFP / Abdelhak Senna
Matangazo ya kibiashara

Rais mpya wa marekani alisaini agizo rasmi la rais linaofuta ufadhili na fedha za mashirika ya kimataifa yasio ya kiserikali zinazotumiwa kwa kutoa mimba au yanatetea kwa minajili ya kuwepo kwa sheria inayohalalisha utoaji mimba.

Agizo hilo linalojulikana kama "Global Gag Rule" lilichukuliwa na Rais Ronald Reagan mwaka 1984, lakini lilifutwa na Rais kutoka chama cha Demokratic, Bill Clinton, na kurejeshwa upya narais George W. Bush kutoka cham acha Republican, kisha kufutwa tena na Rais Barack Obama kutoka chama cha Democratic.

Uamuzi huo unakuja siku mbili baada ya mfululizo wa maandamano ya wanawake duniani kwa ajili ya kutetea haki zao.

Nchini Kenya, angalau hospitali nyingi ambazo ni wanachama wa Shirikisho la Kimataifa la Uzazi wa Mpango (IPFF) ztaathirika na uamuzi wa Donald Trump.

Rais wa Marekani Donald Trump alitia saini agizo rasmi la rais kupiga marufuku kutolewa kwa pesa za serikali ya Marekani kufadhili mashirika ya nchi za nje ambayo yanatekeleza au kutoa habari kuhusu utoaji mimba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.