Pata taarifa kuu
MAREKANI-CUBA-USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Barack Obama awasili Cuba kwa ziara ya kihistoria

Rais wa Marekani amewasili nchini Cuba Jumapili Machi 20 ili kuidhinisha uhusiano kati ya Washington na Havana uliofufuliwa hivi karibuni, baada ya zaidi ya miongo mitano ya uhasama. tukio la kihistoria.

Rais Obama atembea na familia yake katika mitaa ya Havane.
Rais Obama atembea na familia yake katika mitaa ya Havane. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mwanahabari wetu anne Marie Capemaccio, Barack Obama na familia yake wamewasili huku mvuanyingi zikinyesha siku ya Jumapili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Havana, ziara muhinu kwa mujibu wa raia wa Cuba. Rais wa Marekani ameweka mguu wake katika ardhi ya Cuba, tukio ambalo limerushwa hewani moja kwa moja kwenye runinga ya taifa. Na katika mitaa ya mji mkuu, watu wengi wamekua wakitazama televisheni katika migahawa na nyumani kwao. Mayowe yalipigwa kwa sauti kubwa, Rais wa Marekani alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Havana.

"¿Que bola Cuba?" ("habari yako Cuba? "), amesema Barack Obama kwenye Twitter alipowasili, akitumia maneno maarufu.

Familia ya rais imetembelea Kanisa kuu ya Havana katika mji mkongwe, uliopigwa marufuku kwa umma kwa masaa machache, huku akiambatana na Kardinali Jaime Ortega. Pamoja na hali mbaya ya hewa, watalii wengi na raia wa Cuba walitaka kuja kumuona kwa macho yao wenyewe rais wa Marekani. Clara, raia wa Cub, mwenye umri wa miaka arobaini, hakutaka kwa lolote kukosa kushuhudia tokio hili la kihistoria.

Muda mfupi kabla kupumzika, Barack Obama amemsifu Kiongozi wa Ujumbe wa Marekani nchini Cuba, Jeffrey DeLaurentis, mmoja wa wasanifu wa muungano huu. Pengine DeLaurentis hatateuliwa kuwa balozi chini ya utawala wa Rais Obama kwa sababu Baraza la Seneti linapaswa kupitisha uteuzi huo na Wabunge wa chama cha Republican, wanaopinga muungano huo, wametangaza kukataa kushughulikia faili hiyo. Lakini kila mtu amesikia Jumapili hii katika mji wa Havana Rais Obama akimpongeza balozi DeLaurentis na timu yake kwa ajili ya kazi zao.

Mkutano na Raul Castro Jumatatu

Mambo muhimu yataanza tu siku ya Jumatatu. Barack Obama na Raul Castro watakutana saa 10 asubuhi (saa za Cuba), ili waende wote pamoja katika eneo la kumbukumbu, alikozikwa Jose Marti, shujaa wa taifa, mshairi, mwanasiasa, mwanafalsafa, anayechukuliwa kama baba wa mapinduzi ya Cuba. Rais wa Marekani ataweka shada la maua kwenye kaburi hilo.

Baada ya picha rasmi, pichaambayo itawekwa katika historia ya Cuba, Raul Castro na Barack Obama watakutana kwa mazungumzo yatakayodumu masaa mawili kabla ya kutoa tangazo la pamoja kwa vyombo vya habari. White House ikua ilisema kuwa kutakua na mkutano na waandishi wa habari, lakini ni wazi kikao cha maswali cha waandishi wa habari kimekataliwa na itifaki ya Cuba.

Siku ya leo itaendelea kwa mazungumzo kati ya Rais wa Marekani na wajasiriamali wa nchi zote mbili. Kunatarajiwa matangazo na masoko mapya.

Siku hii itamalizika kwa chakula cha jioni katika Ikulu ya Mapinduzi. Obama na familia wamealikwa na Raul Castro.

Jumanne, Barack Obama atakutana na wapinzani wa serikali ya Cuba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.