Pata taarifa kuu
MAREKANI - UCHUMI

Mkuu wa hazina aonya kuhusu uchumi wa Marekani

Mkuu wa hazina ya Marekani, Janet Yellen ameonya kuwa uchumi wa Marekani unakabiliwa na hali ngumu ya mapato ya ndani pamoja na mdororo wa kiuchumi unaoikabili dunia kwa sasa.

Mkuu wa hazina nchini Marekani Janet Yellen
Mkuu wa hazina nchini Marekani Janet Yellen REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kwa umakini mkubwa ukilinganisha na alivyozungumza mwezi December mwaka jana wakati akitoa tathmini ya uchumi wa taifa lake, safari hii, Yellen ameonekana kuguswa na namna mambo yanavyoenda na kuongeza kuwa huenda riba kwenye mabenko ikaongezeka ili kukabiliana na changamoto ya kiuchumi.

Yellen amesema kuwa hali tete ya kifedha inayoikabili nchi yake imetokana na uchumi wake kutokuwa kwa wakati, ukopaji mkubwa na kutothaminiwa kwa thaman ya dola.

Yellen ameendelea kusema kuwa hali ya uchumi haikuwi nchini Marekani kutokana na kukosekana kwa hatuwa za kudhibiti upandaji wa bei, ukopaji mkubwa pamoja na kushnuka kwa thamani ya dola.

Hali hiyo amesema inaweza kuwa mbaya zaidi iwapo hali hii haitobadilika, kwani inaweza kuathiri sekta ya ajira, licha ya kwamba kushuka kwa nei ya mafuta kunaweza kufidia.

Yellen kwenye taarifa yake amesema kuwa hali hiyo huenda ikasababisha taifa hilo kujikuta kwenye hali tetet ya kifedha na uchumi wake kuathirika kwenye soko la dunia, kama ilivyoshuhudiwa mwaka mmoja uliopita.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.