Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI

wapinzani wa utawala wa Washington washinda katika jimbo la New Hampshire

Kinara wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump na mwenzake wa Democrat. Bernie Sanders wamefanikiwa kushinda kwenye uchaguzi wa awali wa jimbo la New Hampshire, uchaguzi ambao umekuwa wa upinzani mkali na kushuhudia wagombea wanaopinga utawala wa washington wakipita kwa kishindo.

Donald Trump, januari 26 akiwa katika kampeni kwenye chuo cha Iowa
Donald Trump, januari 26 akiwa katika kampeni kwenye chuo cha Iowa REUTERS/Scott Morgan
Matangazo ya kibiashara

Ushindi wa Trump kwenye jimbo hili umemuongezea nguvu kwenye kampeni zake baada ya kuanguka vibaya kwenye uchaguzi wa jimbo la Iowa juma liliopita dhidi ya mpinzani wake Seneta Ted Cruz.

Hillary Clinton wa Democrat ambaye alipata ushindi finyu dhidi ya Sanders kwenye jimbo la Iowa, amempongeza mpinzani wake na kukubalia kushindwa kwenye jimbo la New Hampshire lakini ameahidi kupambana zaidi kupata kura za vijana ambao walimpigia kura seneta Sanders.

Kwa upande wake, Bernie Sanders, licha ya kumpongeza Clinton kwa kampeni za nguvu, amesema idadi ya kura alizopata ni historia kwenye kampeni zake na sasa ni wazi umemsafishia njia ya kuelekea ikuli, na kuongeza kuwa matajiri waliotumia fedha nyingi kwenye kampeni zao wameonekana kushindwa.

Ushindi wa Trump na Sanders kwenye jimbo la New Hampshire, ulitabiriwa na vyombo vingi vya habari, kwa kile ambacho kimeelezwa kuwa vijana wengi kutoka kambi zote wanauwanga mkono wagombea hao.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.