Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN-USHIRIKIANO

Washington yawasiliana na Tehran kuhusu hatima ya mabaharia wake 10

Marekani imekuwa ikiwasiliana na Iran juu ya hatima ya meli mbili za Marekani katika bahari ya Ghuba pamoja na watu 10 ambao wamo katika meli hizo, ambapo Tehran imethibitisha kuwa mabaharia hao wa Marekani wataweza "haraka" kuendelea na safari yao, alisema afisa mmoja wa Marekani.

Picha iliyotengenezwa Novemba 8, 2013 mjini Paris inaonyesha Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry (kulia) na mwenzake wa Iran Javad Zarif (kushoto).
Picha iliyotengenezwa Novemba 8, 2013 mjini Paris inaonyesha Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry (kulia) na mwenzake wa Iran Javad Zarif (kushoto). AFP/AFP/
Matangazo ya kibiashara

"Mapema Jumanne mchana, tumepoteza mawasiliano na meli mbili ndogo za kijeshi ambazo zimekua kisafiri kati ya Kuwait na Bahrain. Tumekuwa na mawasiliano na viongozi wa Iran ambao wametufahamisha kwamba wafanyakazi wetu wako salama", afisa wa Marekani ambaye hakutaka kutaja jina lake, ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP, bila hata hivyo kusema nini kilichotokea kwa meli hizo mbili.

"Tumepokea hakikisho kwamba mabaharia wataruhusiwa haraka kuendelea na safari yao", chanzo hicho kimeongeza.
Kwa mujibu wa afisa mwingine wa Marekani, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amewasiliana kwenye simu na mwenzake wa Iran Mohammad Javad Zarif.

Tangazo hilo limekuja saa chache kabla ya hotuba kuhusu muungano wa Rais Barack Obama ambapo atafutilia mbali vipaumbele vyake katika suala la sera ya ndani, lakini pia sera za kigeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.