Pata taarifa kuu
IRAN-NYUKLIA-USALAMA-DIPLOMASIA

Iran yahamishia uranium Urusi, chini ya mpango wa nyuklia

Jumatatu hii Desemba 28, Iran imehamishia kiwango kikubwa cha uranium nchini Urusi, hatua muhimu katika makubaliano ya kihistoria juu ya mpango wake wa nyuklia ulioafikiwa na nchi zenye nguvu msimu uliopita.

Rais wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) akipeana mkono na mwenzake wa Iran Hassan Rouhani Wakati mkutano na waandishi wa habari baada ya mazungumzo mjini Tehran, Iran, Novemba 23, 2015.
Rais wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) akipeana mkono na mwenzake wa Iran Hassan Rouhani Wakati mkutano na waandishi wa habari baada ya mazungumzo mjini Tehran, Iran, Novemba 23, 2015. REUTERS/Alexei Druzhinin/Sputnik/Kremlin
Matangazo ya kibiashara

Marekani imekaribishwa uamzi huo wa Iran uliotajwa na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry wenye "mafanikio makubwa" kuelekea utekelezaji wa makubaliano ya kuizuia Tehran kupata silaha za nyuklia.

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imethibitisha mchakato huo. Mkuu wa mpango wa nyuklia wa Iran Ali Akbar Salehi ameliambia shirika la habari la Iran ISNA kwamba "mchakato wa kuhamisha mafuta umefanyika."

Likizungumzia vyanzo vya Iran na vya Urusi visiokua rasmi, shirika la habari la Iran ISNA limesema kuwa "kiwango cha uranium kiliohamishiwa nchini Urusi kimezidi tani 8.5 na Iran imepokea, katika kubadilishana bidhaa hiyo, tani 140 za uranium asilia."

Chini ya makubaliano yaliyofikiwa katika mji wa Vienna mwezi Julai kati ya Iran na nchi sita zenye nguvu duniani, Iran ilijikubalisha kutomiliki zaidi ya kilo 300 za nyenzo hizo wakati wautekelezaji wa Mkataba.

Hivyo, Tehran haina mafuta ya kutosha kwa ajili ya kuimarisha ngazi muhimu kwa kutengeneza silaha za nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.