Pata taarifa kuu
ARGENTINA-KUAPISHWA-SIASA

Argentina: Maelfu ya wafuasi "wamuaga" Cristina Kirchner

Maelfu ya wafuasi wa rais wa Argentina wamekusanyika Jumatano nje ya ukumbi wa Ikulu ya rais katika mji wa Buenos Aires ili kumsabahi na kumuaga Cristina Kirchner, ambaye anaondoka madarakani baada ya mihula miwili ya miaka 4.

Wafuasi wakija kumuaga na kusema "asante" Cristina Kirchner, mbele ya ukumbi wa Ikulu ya rais katika mji wa Buenos Aires, Desemba 9, 2015.
Wafuasi wakija kumuaga na kusema "asante" Cristina Kirchner, mbele ya ukumbi wa Ikulu ya rais katika mji wa Buenos Aires, Desemba 9, 2015. REUTERS/Andres Stapff
Matangazo ya kibiashara

Mapema Jumatano jioni, Cristina Kirchner angelihotubia umati wa watu.

Alhamisi hii, Mauricio Macri atamrithi na kuapishwa kuwa rais. Meya wa mji wa Buenos Aires kutoka chama cha mrengo wa kati kulia alishinda uchaguzi wa urais dhidi ya Daniel Scioli, mgombea wa muungano wa vyama vya mrengo wa kushoto madarakani.

Sera ya utawala wa Kirchner imepata pigo kubwa Jumanne wiki hii wakati ambapo vyombo vya sheria, baada ya Bw. Macri kuwasilisha malalamiko yake, vilitatua mzozo juu ya suala kukabidhiana madaraka, na kuamuru Bi Kirchner kuondoka ikulu Jumatano usiku.

Katika mshikamano na rais, vyama vya upinzani vinavyomuunga mkono Kirchner vimesema Jumatano wiki hii kuwa havitokuwepo bungeni wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo.

Wabunge kutoka chama cha Kirchner wana nguvu katika baraza la wawakilishi na ni wengi katika Baraza la Seneti.

Cristina Kirchner, mwenye umri wa miaka 62, hangeweza kuwania muhula wa wa tatu mfululizo, lakini anaweza kuwania tena mwaka 2019.

Bibi Kirchner angelipaswa kuondoka mji mkuu wa Argentina Alhamisi hii na kujielekeza katika ngome yake ya Patagonia kuhudhuria sherehe ya kukabidhiwa madaraka ya uongozi dada wa mume wake, Alicia Kirchner, ambaye alichaguliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Santa Cruz.

Marais wengi au au wakuu wa wajumbe wa kigeni, kama vile Rais wa zamani wa baraza la Seneti Jean-Pierre Bel upande wa Ufaransa, walianza kuwasili Jumatano katika mji mkuu wa Argentina. Marais kadhaa wanatarajiwa kuwasili Alhamisi hii kwa ajili ya sherehe ya kuapishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.