Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KUSINI-SHAMBULIO-USALAMA

Balozi wa Marekani ashambuliwa Seoul

Balozi wa Marekani nchini Korea Kusini Mark Lippert, ameshambuliwa na kudungwa kisu usoni na mkononi jijini Seoul.

Rais wa Marekani Barack Obama akieleze kusononeshwa na tukio lililomtokea balozi wake katika mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul.
Rais wa Marekani Barack Obama akieleze kusononeshwa na tukio lililomtokea balozi wake katika mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Lippert mwenye umri wa miaka 42, alishambuliwa wakati akihudhuria dhifa ya kiamsha kinywa na wadau mbalimbali wa sanaa jijini Seoul.

Ripoti zinasema kuwa Balozi huyo alikimbizwa hospitalini baada ya shambulizi hilo na anaendelea vizuri.

Polisi wamesema, mtu aliyemshambulia Balozi huyo wa Marekani ni mwanaume mwenye umri wa miaka 55 anayehusishwa na maswala ya uanaharakati ambaye wakati akitenda kitendo hicho alisikika akisema, Korea Kusini na Korea Kaskazini zinastahili kuwa nchi moja.

Mvamizi huyo ambaye amekamatwa na polisi pia alisikika akipinga mazoezi ya kijeshi yanayoendelea kati ya wanajeshi wa Korea Kusini na Marekani nchini humo.

Rais wa Marekani Barrack Obama amempigia simu balozi wake na kumtakia nafuu ya haraka na kulaani kitendo hicho cha kushambuliwa kwa balozi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.