Pata taarifa kuu
HAITI-AJALI-VIFO-USALAMA

Watu zadi ya 10 wamefariki katika tamasha Haiti

Nchini Haiti, kwa usiku wa pili wa tamasha la kitaifa limemalizika huku kukiwa na watu waliofariki. Watu zaidi ya kumi wamefariki kutokana na kukanyagana.

Nchini Haiti, kama ilivyo katika nchi nyingi tamasha hugubikwa na aina mbalimbali za michezo. Port-au-Prince tarehe 15 Februari mwaka 2015.
Nchini Haiti, kama ilivyo katika nchi nyingi tamasha hugubikwa na aina mbalimbali za michezo. Port-au-Prince tarehe 15 Februari mwaka 2015. REUTERS/Andres Martinez Casares
Matangazo ya kibiashara

Ajali hii imetokea katika eneo liitwalo "Champ de Mars", ambapo maelfu ya watu walikuwa wamekusanyika kwa kucheza katika gwaride.

Kwa mujibu wa mwanahabari wa RFI katika mji wa Port-au-Prince, Amélie Baron, tukio hilo lilitokea muda mfupi kabla ya saa tisa alfajiri kwenye eneo la Champ de Mars, katikati mwa mji mkuu wa Haiti.

Mmoja kati mwimbaji wa kundi maarufu la Hip Hop Barikad Crew alikuwa amesimama juu ya mashua, wakati aliteleza, huku kichwa chake kikivuta waya ya umeme ambayo ilikatika na kusababisha ajali.

Mwimbaji huyo alianguka nyuma ya mashua na kupigwa na umeme, jambo ambalo lilisababisha wimbi kubwa la hofu miongoni mwa wale waliokuwa juu ya mashua hiyo na umati wa watu waliokuwa wamekusanyika pembezoni mwa gwaride hilo. Mwimbaji huyo amelazwa hospitalini na yuko katika hali ya maututi.

Hali hii ya kukanyagana imesababisha vifo vya watu zaidi ya 10. Wizara ya Mawasiliano ya Haiti pia imetaja kuwa watu arobaini wamejeruhiwa, huku ikibaini kwamba idadi hii ni ya muda.

Mchezo huu ni tukio la kwanza la kitamaduni nchini Haiti. Wakati huohuo, rais wa Haiti, Michel Martelly, ametoa rambirambi zake kwa familia ziliyowapoteza ndugu zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.