Pata taarifa kuu
ARGENTINA-MAUAJI-SHERIA-SIASA

Kifo cha Alberto Nisman chazua hisia tofauti

Taarifa kutoka Argentina zinasema mwendesha mashtaka maarufu nchini humo aliyepatikana amefariki ndani ya nyumba yake mjini Buenos Aires, Alberto Nisman alikuwa ameandika barua ya kukamatwa kwa rais wa nchi hiyo Cristina Fernandez.

Mwendesha mashitaka maarufu Alberto Nisman, mwezi Mei mwaka 2013.
Mwendesha mashitaka maarufu Alberto Nisman, mwezi Mei mwaka 2013. REUTERS/Marcis Brindicci/Files
Matangazo ya kibiashara

Alberto Nisman alimtuhumu rais huyo kuzuia uchunguzi wa mashambulio mabaya zaidi ya ugaidi kuwahi kufanyika nchini Argentina.

Alberto Nisman alikuwa amepangiwa kutoa maelezo ya kina kwa bunge la taifa hilo.
Alberto Nisman alikuwa akisimamia uchunguzi kuhusiana na mlipuko katika kituo kimoja cha kijamii kilichokuwa kikisimamiwa na Wayahudi mjini Buenos miaka 20 iliyopita ambapo watu watano waliuwawa.

Nisman alimshutumu Rais Fernandez na wakuu wengine kwa kuzuia uchunguzi huo.

Mwezi Juni 2014, alikuwa aliomba rais Cristina Kirchner azuiliwe kwa lengo la kuendelea na uchunguzi. Alberto Nisman alikutwa amefariki katika mazingira ya kutatanisha tarehe 18 Januari mwaka.

Siku nne kabla ya kifo chake, mwendesha aliye kua akichunguza kuhusu mashambulizi hayo dhidi ya Wayahudi yaliyosababisha vifo vya watu 85 mwaka 1994 - amelimtuhumu Kirchner, akisema kuwa hakutoa nafasi ya kuwahukumu washukiwa wa madshambulizo hayo ambao ni raia wa Iran.

Maandamano ya raia katika mji mkuu wa Argentina, Buenos Aires, Januari 21 mwaka 2015 wakiomba ukweli kuhusu kifo cha kutatanisha cha mwendesha mashitaka maarufu Alberto Nisman.
Maandamano ya raia katika mji mkuu wa Argentina, Buenos Aires, Januari 21 mwaka 2015 wakiomba ukweli kuhusu kifo cha kutatanisha cha mwendesha mashitaka maarufu Alberto Nisman. REUTERS/Marcos Brindicci

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.