Pata taarifa kuu
BRAZIL-Kuapishwa-Siasa

Dilma Roussef aapishwa kuwa rais wa Brazil

Dilma Rousseff amepishwa kuongoza nchi ya Brazil kwa muhula wa pili baada ya kushinda urais mwaka uliopita.

Dilma Rousseff, amepishwa kuongoza nchi ya Brazil kwa muhula wa pili baada ya kushinda urais mwaka uliopita.
Dilma Rousseff, amepishwa kuongoza nchi ya Brazil kwa muhula wa pili baada ya kushinda urais mwaka uliopita. REUTERS/Ueslei Marcelino
Matangazo ya kibiashara

Rais Rouseff ameahidi kupambana na ufisadi na kuimarisha uchumi wa nchi hiyo kwa kipindi cha miaka minne atakapokuwa madarakani.

Mpiganaji huyo wa zamani wa msituni amesisitiza kuwa serikali yake haitafumbia macho vitendo viovu na atamwadhibu yeyote atakayebainika kuhusika na ufisadi nchini humo.

Sherehe ya kumwapisha rais Rouseff zilifanyika jijini Brasilia na kulishuhudiwa katika sherehe hizo Makamu wa rais wa China na Marekani pamoja na marais 13 kutoka mataifa ya Latin America.

Rais Rouseff alipata ushindi mwembamba wakati wa uchaguzi wa mzunguko wa pili mwezi Oktoba mwaka jana katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa.

Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema, kilichomsaidia Bi. Rouseff kushinda uchaguzi ni ukaraibu na wananchi wa kawaida na kuzindua miradi na kuimarsiha maisha ya wananchi wa kiwango cha chini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.