Pata taarifa kuu
MEXICO-Haki za binadamu-Usalama

Makaburi 6 ya pamoja yagunduliwa Mexico

Watu wawili wamekiri kutekeleza mauaji ya watu 17 miongoni mwa wanafunzi 43 wa chuo kikuu ambao hawajulikani waliko tangu siku nane zilizopita baada ya makabiliano makali kati ya wanafunzi hao na polisi wakati wa maandamano.

Wanajeshi wakiwa katika eneo ambako makaburi 6 ya pamoja yamegunduliwa.
Wanajeshi wakiwa katika eneo ambako makaburi 6 ya pamoja yamegunduliwa. REUTERS/Jorge Dan Lopez
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa wiki hii, miili 28 ilikutwa katika makaburi sita ya pamoja yaliyogundua karibu na eneo la Iguala katika jimbo la Guerrero.

Jinsi wakati unavyoenda, ndivyo familia 43 za wanafuzi hao zinaendelea kuwa na dhiki na kukata tamaa kwa kuwaona tena ndugu zao. Utata umeibuka kati ya familia hizo na serikali, ambapo familia zimeitaka serikali kutoa taarifa haraka iwezekanavyo kuhusu miili iliyokutwa katika makaburi ya siri, huku zikiwa na hofu kwamba miili hio ni ya ndugu zao.

Jana Jumapili ndugu, jama na marafiki wa wanafunzi hao wakiwa pamoja na wanafunzi wa chuo kikuu cha waalimu katika jimbo la Guerrero walizuia barabara kuu inayotokea katika mji wa Mexico kuelekea Guerrero ili kuishinikiza serikali kutoa taarifa zaidi kuhusu miili hiyo ilikutwa katika makaburi ya pamoja.

Hata hivo familia hizo zitalazimika kusubiri kati ya siku 15 na miezi miwili kabla ya serikali kujua uraia na majina ya watu hao waliouawa. Baadhi ya miili ya watu hao imeshaharibika. Vipimo vya damu vimeanzishwa ili kujua iwapo marehemu hao walikua na uhusiano wa kidugu na watu hao wanaoishinikiza serikali kutoa majina ya watu hao.

Makaburi hayo ya siri yaligunduliwa baada ya watu wawili waliokiri kuwauawa wanafunzi 17 kuhojiwa, wakibaini kwamba walipewa amri na mkuu wa polisi wa kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya. Kukiri kwa watu hao wawili kumepelea watu zaidi ya thelathini wakiwemo askari polisi 22 kukamatwa.

Askari polisi hao wanatuhumiwa kuwaua wanafunzi 3 wa chuo kikuu waliokua wakiandamana katika mji wa Iguala, na kuwashikilia wengine zaidi ya arobaini, kwa amri ya mkuu wa kikosi cha usalama wa umma katika mji wa Iguala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.