Pata taarifa kuu
BRAZIL-Uchaguzi-Siasa

Brazil: matokeo ya uchaguzi yasubiriwa

Baadhi ya wapiga kura milioni 142 nchini Brazil wameshiriki leo Jumapili Oktapba 5 uchaguzi , ambapo kura tano zimepigwa kwa chaguzi mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa rais na wabunge.

Mtoto akichezea kadi za kupigia kura nje ya kituo cha kupigia kura katika kitongoji cha mji wa Rio de Janeiro, Oktoba 5 mwaka 2014.
Mtoto akichezea kadi za kupigia kura nje ya kituo cha kupigia kura katika kitongoji cha mji wa Rio de Janeiro, Oktoba 5 mwaka 2014. REUTERS/Ricardo Moraes
Matangazo ya kibiashara

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa saa 11:00 (Saa zakimataifa) na vitafungwa saa sita usiku (saa za kimataifa). Kila mpiga kura, ambaye ana wajibu wa kupiga kura, anatakiwa kuwauchagua wabunge wa kikanda, magavana, theluthi moja ya maseneta lakini pia rais wa baadaye . Wagombea kuu kwenye kiti cha raisa ni watatukwa, Dilma Rousseff, Marina Silva na Aecio Neves, ambao wamepiga kura.

Dilma Rousseff, ambaye amepewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo, na kuliongoza kwa muhula wa pili taifa hilo la Brazil, amejielekeza kusini mwa Brazili katika mji wa Porto Alegre ambako amepigia kura.

Akihojiwa na waandishi wa habari, Dilma Roussef amesema, uchaguzi huo ni silaha inayoshikiliwa na raia wa Brazil ambao wanakabiliwa na umasikini. Mgombea wa chama cha wafanyakazi amekua akikumbusha katika kampeni zake za uchaguzi kwamba akibahatika kuchaguliwa, atapambana na umasikini unaowakabili raia.

Wapinzani wawili wa Roussef, ambao wot ni kutoka chama cha kisoshalisti wamepigia kura katika majimbo yao. Marina Silva amepigia kura katika jimbo la Acre, kaskazini mwa Brazil, na baadaye amejielekeza Katika mji wa kiuchumi wa Saõ Paulo, unaopatikana kwa mwendo wa ndege wa saa tautu na mji mkuu wa Brazil.

Baada ya kupiga kura, mgombea wa tatu. Aecio Neves, ametembela eneo alikozaliwa la Minas Gerais (kusini mashariki) ambako ni makao mkuu ya upinzani.

Matokeo ya mwanzo yanatazamiwa kutolewa saa nne usiku (saa za kimataifa).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.