Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFGHANISTAN

Mwanajeshi wa Marekani aachiwa huru nchini Afghanistan baada ya miaka mitano

Mwanajeshi wa Marekani aliyekuwa akishikiliwa nchini Afghanistani ameachiwa jana Jumamosi kwa kubadilishana na wafungwa watano wa kundi la Taliban waliokuwa wanazuiliwa katika gereza la Guantanamo Bay, katika mpango mkubwa ulioandaliwa na Qatar. 

Sajenti Bowe Bergdahl, aliyetekwa nyara na waasi wa Taliban mwaka 2009,
Sajenti Bowe Bergdahl, aliyetekwa nyara na waasi wa Taliban mwaka 2009, AFP PHOTO HANDOUT-INTELCENTER"
Matangazo ya kibiashara

Sajenti wa jeshi la Marekani Bowe Bergdahl ambaye alikamatwa karibu miaka mitano iliyopita alikuwa katika hali nzuri baada ya wapiganaji wa Taliban kumkabidhi kwa maafisa kadhaa wa vikosi vya operesheni maalumu za Marekani waliosaidiwa na helikopta kufika katika eneo la mafichoni mashariki mwa Afghanistan, viongozi wa usalama wamesema.

Kwa upande wa wafungwa watano wa Taliban wamesafirishwa hadi Qatar ambako vikwazo vitawekwa dhidi ya harakati na shughuli zao, afisa wa Marekani amesema.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.