Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-MAREKANI

Kundi la Taliban lafanya shambulizi la kulipiza kisasi kwa kuchomwa Quran Tukufu

Watu tisa wameuawa na wengine kumi wakijeruhiwa kwenye shambulizi la bomu la kujitoa mhanga lililotekelezwa na Mfuasi wa Kundi la Wanamgambo wa Taliban Mashariki mwa Afghanistan katika Jiji la Jalalabad.

Shambulizi la bomu lililotekelezwa na Kundi la Wanamgambo wa Taliban katika Uwanja wa Ndege huko Jalalabad
Shambulizi la bomu lililotekelezwa na Kundi la Wanamgambo wa Taliban katika Uwanja wa Ndege huko Jalalabad
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo limetekelezwa katika Uwanja wa Ndega uliopo Mashariki mwa Afghansitan na tayari tukio hilo limehusishwa na kitendo cha Wanajeshi wa Marekani waliopo kwenye Jeshi la Kujihami la Nchi za Magharibi NATO kuchoma Quran Tukufu.

Majeshi ya NATO yamesema hakuna taarifa zozote zilizothibitisha kama kuna mwanajeshi yoyote kutoka nchi za kigeni ambaye amepoteza maisha kwenye shambulizi hilo lililopangwa na kutekelezwa na Kundi la Taliban.

Msemaji wa Kundi la Wanamgambo wa Taliban Zabiullah Mujahid kupitia email aliyotuma kwenye vyombo mbalimbali vya habari amesema kuwa shambulizi hili ni la kiulipiza kisasi kwa kile kichofanywa na majeshi ya Marekani kwa kuchoma moto Quran Tukufu.

Mashuhuda wa Tukio hili wanasema kuwa magari manne yameharibiwa vibaya kwenye geti la kuingilia Uwanja wa Ndege sehemu ambayo mshambuliaji wa kujitoa mhanga alitekeleza shambulizi lake.

Tangu kuibuka kwa taarifa za kuchomwa moto Quran Tukufu na wanajeshi wa Marekani hapo juma lililopita nchi ya Afghanistan imeshuhudia machafuko na ghasia ambazo zimechangia vifo vya watu zaidi ya kumi.

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai amekuwa mstari wa mbele kulaani kile ambacho kimefanywa na majeshi ya Marekani na hata siku ya jumapili aliendelea na msimamo wake alipohutubia kupitia Televisheni.

Viongozi wa NATO pamoja na Rais wa Marekani Barack Obama kwa nyakati tofauti wameomba radhi kwa kile ambacho kimetokea wakati huu ambapo uchunguzi wa kina ukiendelea kufanyika.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.