Pata taarifa kuu
Marekani-Venezuela

Serikali ya Washington yakanusha taarifa za kumkatalia rais wa Venezuela kutumia anga lake

Serikali ya Marekani imekanusha taarifa za kumzuwia rais wa Venezuela Nicolas Maduro kutumia anga yake katika ziara yake kuelekea nchini China inayo tarajiwa kufanyika hapo kesho Jumamosi. Naibu msemaji wa serikali ya Marekani Marie Harf amesema, serikali ya Washington imeruhusu viongozi wa Venezuela kutumia anga ya Marekani.

Naibu msemaji wa Serikali ya Marekani Marie Harf
Naibu msemaji wa Serikali ya Marekani Marie Harf
Matangazo ya kibiashara

Naibu msemaji huyo ameeleza kuwa licha ya kwamba ombi la kutumia anga ya Marekani halikuheshimu taratibu na sheria za Marekani, viongozi wa Marekani wanashirikiana na wanadiplomasia wa Venezuela nchini humo kujaribu kutatua tatizo hilo.

kulingana na taarifa hiyo, ombi la serikali ya Caracas la kutaka kutumia anga ya Marekani lilitolewa siku moja kabla ya kutekelezwa badala ya siku tatu kama ilivyo katika sheria na utaratibu wa Marekani, ambapo pia ndege hiyo sio ndege ya serikali kama ilivyo katika utaratibu wa kidiplomasia

Marie Harf amesema viongozi wa Marekani wanahakikisha swala hilo linapatiwa ufumbuzi katika saa chache zijazo, na tayari wamewafahamisha viongozi wa Venezuela kuhusu utaratibu wa ombi kama hilo la kidiplomasia na tayari wamewapa taarifa ya kumtumia anga hiyo ya Marekani.

Hapo jana waziri wa mambo ya nje wa Venezuela alifahamisha kwamba Marekani imemkatalia rais Maduro kutumia anga ya Marekani na kuchukulia kitendo hicho kama kashfa kubwa dhidi ya taifa lake.

Maduro alitangaza tangu jumanne kwamba ataelekea jijini Pekin Septemba 21 na 24 kukutana na mwenziwe wa nchi hiyo Xi Jinping katika dhamira ya kudumisha uhusiano wa kistrategia

Washington na Caracas ambazo hazina uhusiano wa kaidiplomasia tangu mwaka 2010, zimekuwa zikivutana tangu kipindi kadhaa.

Serikali ya hayati Hugo Chavez 1999-2013 na hii mpya ilioko sasa ya Nicolas Maduro zimekuwa zikiituhumu Marekani kuw ana mpango wa kuyumbisha usalama wa taifa hilo kupitia wapinzani wa serikali iliopo madarakani.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.