Pata taarifa kuu
BRAZIL-MAANDAMANO

Rais wa Brazili Dilma Rouseff apeleka mapendekezo ya kura za maoni bungeni

Serikali ya Rais wa Brazili Dilma Rouseff imepeleka mapendekezo yake bungeni hapo jana, ya kutaka kufanyika kwa kura ya maoni juu ya mabadiliko ya kisiasa.

REUTERS/Ueslei Marcelino
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya maandamano ya majuma matatu kupinga vitendo vya rushwa na matumizi makubwa kwa ajili ya michuano ya Kombe la mabara halikadhalika mashindano yajayo ya Kombe la dunia ambayo yatafanyika nchini humo.
 

Mapendekezo haya yaliwasilishwa kwa Kiongozi wa Baraza la Senet na Bunge, Renan Calheiros , huku waziri wa Sheria, Jose Eduardo Cardozo ametangaza kuwa atafanyia kazi maombi ya Rais Rouseff ili kama kutakuwa na mabadiliko kutokana na kura ya maoni yaanze kufanyiwa kazi kuanzia Mwezi Oktoba mwaka 2014 mwaka mmoja baada ya uchaguzi wa Rais.
 

Cardozo amesema kura ya maoni itazingatia mabadiliko katika Kampeni za uchaguzi, mfumo wa upigaji kura za ubunge, sheria za kusimamia muungano wa vyama na kura za siri za wabunge.
 

Takriban Raia wa Brazil milioni 1.5 waliingia mtaani kupinga kupanda kwa nauli na huduma nyingine za kijamii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.