Pata taarifa kuu
Venezuela

Mahakama ya nchini Venezuela yatarajiwa kusogezwa mbele kwa Tarehe ya kuapishwa kwa Rais Hugo Chavez

Ikiwa ni saa chache toka mahakama kuu nchini Venezuela kuthibitisha na kukubali kusogezwa mbele kwa tarehe ya sherehe za kuapishwa kwa rais wa nchi hiyo Hugo Chavez upinzani nchini humo umeendelea kusisitiza kuwa hatua hiyo imeenda kinyume na katiba ya nchi.

Rais wa Venezuela, Hugo Chavez
Rais wa Venezuela, Hugo Chavez AFP/Juan BARRETO
Matangazo ya kibiashara

Henrique Capriles ambaye ni kiongozi mkuu wa upinzani aliyechuana kwenye kinyang'anyiro cha urais na Rais Chavez amekubaliana na uamuzi wa mahakama licha ya kutaka madaraka ya rais kwasasa yakabidhiwe kwa makamu wa Rais Nicolas Maduro.

Kauli yake imeonekena kukinzana na ile ya baadhi ya Wanasheria na Mawaziri wa Serikali ambapo wanataka kutafsiriwa vizuri kwa katiba ya nchi.

Hii leo wafuasi wa rais Chavez wanatarajiwa kufanya maandamano ya nchi nzima kumuunga mkono kiongozi wao ambaye anaendelea kupatiwa matibabu ya saratani nchini Cuba.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.